GET /api/v0.1/hansard/entries/679197/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 679197,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/679197/?format=api",
    "text_counter": 257,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "Nakushukuru sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Hata mimi sitaki kuachwa nyuma kukupongeza kwa wadhifa huu mpya uliopewa. Naongea kama mtu ambaye amekusikiliza ukihudumu. Najua utaweza hiyo kazi. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Naomba Serikali iangalie haya mambo ya maji vile iliangalia mambo ya stima. Ijapokuwa mradi wa stima ni wa kupeleka umeme kwa kila shule ya upili ya umma, kwa karatasi, madhumuni ya pili yalikuwa kupelekea wananchi stima. Hii ni kwa sababu kama kila shule ya msingi ya umma inapata stima, inawezekana kila sehemu ya nchi itakuwa imepata umeme kufikia sasa. Mradi huu ukichukuliwa hivyo – kuwa kila shule ya msingi ya umma ipelekewe maji – kila sehemu katika nchi hii itapata maji. Kwa hivyo, huu mradi hautakuwa wa kunufaisha wanafunzi tu. Utanufaisha maeneo yote ambayo yamezunguka hizo shule za umma. Pili, ni kweli huduma ya kusambaza maji ni wajibu wa serikali za ugatuzi. Jukumu la Serikali Kuu ni mabwawa makubwa makubwa na miradi mikubwa mikubwa ya maji na kulinda chemichemi za maji. Tunapoongea kuhusu Hoja hii, itakuwa muhimu Serikali iangalie kama kuna uwezekano wa kusambaza maji katika kila mahali. Iwe ni kama vile imefanya mradi huu wa hospitali mbili katika kila kaunti. Ule ni wajibu wa Serikali kuu na sio wa kaunti, Serikali Kuu inaweza kupeana hazina kwa serikali za kaunti ziweze kutimiza wajibu wake, na Serikali kuu iwe ikifanya wajibu wake. Tunataka kuwe na ushirikiano kwa sababu hatutaki tena ugomvi mkubwa. Jinsi Serikali ilivyofanya ratiba nzuri ya kufadhili hospitali mbili katika kila kaunti, inapaswa kufadhili miradi itakayopeleka maji kwa kila shule ya umma. Tukiongea mambo ya maji katika shule za umma, kuna shule ambazo zina mashamba makubwa kuliko wanayohitaji kujenga. Pia kuna shule nyingine zenye miradi ya kujiinua kiuchumi kama ukulima. Shule hizo zikipata maji, watanyunyizia mimea ambayo inafanya vizuri The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}