GET /api/v0.1/hansard/entries/679198/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 679198,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/679198/?format=api",
    "text_counter": 258,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "katika maeneo hayo. Watapata fedha za kufanya mambo mengine badala ya kutegemea Serikali na wazazi kwa pesa ambazo zinatumika katika shule hizo. Nikimalizia, nawaomba wote ambao wanasimamia mambo ya maji. Sisi kama Wabunge siku hizi sio wanachama wa Kamati za Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge, lakini tunaweza kuongea na kamati ambazo ziko ili zimulike shule zote kuhakikisha kuwa maji yanafika huku tukingojea Hoja hii, ambayo nina hakika tutaipitisha, itekelezwe na Serikali. Naomba Kamati ya Utekelezaji katika Bunge hili ichukue Hoja hii itakapopitishwa. Iende haraka haraka kwa wizara zinazohusika na isisitize itekelezwe haraka iwezekanavyo. Naunga mkono."
}