GET /api/v0.1/hansard/entries/679389/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 679389,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/679389/?format=api",
"text_counter": 46,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nami pia niunge mkono Mhe. Mwadime. Kitu ambacho ningependa kutofautiana na Mhe. Ali Wario ni kwamba Sheria iko, lakini tetesi huja baada ya ile sheria iliyowekwa kuwa haitumiki. Hi indio maana watu wa pale huweka tetesi ili waone namna wanaweza kusikizwa. Kwa hivyo, ni vizuri vile Mbunge waVoi Mhe. Mwadime amezungumzia juu ya tetesi za wanyama pori ili kuhakikisha kuwa Serikali imepeleka maofisa wakutosha kwa hizo mbuga za wanyama. Inafaa tuangalia sehemu zote ambazo ziko na shida na mambo ya wanyama wapori li ili sehemu hizo zihifadhiwe vizuri. Mhe. Spika, katika nchi hii ya Kenya, wanyama wa pori wanaokaa katika mbuga mara nyingi hutoka na wanadhuru wananchi ambao wanaishi karibu na mbuga hizo. Hata hivyo, Serikali haijahakikisha kwamba wale ambao wameadhirika wamelipwa. Kwa hivyo, ni muhimu Serikali, kupitia tetesi hizi, ihakikishe kwamba yeyote anayeumizwa na mnyama wa pori amelipwa kwa haraka ili maisha yake yaweze kuendelea. Kwa hayo machache, hata mimi ninataka kuwa miongoni mwa wale waliounga mkono tetesi hizi ambazo zimeletwa na Mhe. Mwadime. Nina hakika kamati inayohusika itaweza kuwashughulikia ili watu waVoi wasaidike. Ahsante sana Mhe. Spika."
}