GET /api/v0.1/hansard/entries/679893/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 679893,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/679893/?format=api",
    "text_counter": 550,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mimi pia nachukua fursa hii kuunga mkono Ripoti hii. Tumeona kuwa hali ya mazingira ni muhimu sana katika hali ya maisha ya mwanadamu. Vile vile, tunaona ya kuwa katika mambo haya ya mazingira na ya misitu, kuna mambo mengi ambayo yanasababishwa na mambo haya kama vile vitega maji. Maji ni muhimu katika kila sehemu ya nchi hii. Bila maji, hatuwezi kupata njia ya kukuza vyakula vyetu na mambo mengine. Vile vile, ningependa kusema kwamba nimeunga mkono Ripoti hii na marekebisho yote ya Seneti. Pia, nampongeza mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Amina, kwa kazi nzuri ambayo amefanya. Kama hatungeufanyia Mswada huu marekebisho, basi ingekuwa hali ya “jeke jeke”, kama Waswahili wanavyosema; kwa sababu ingekuwa hatujui mambo yanakuwa namna gani katika mazingira yetu. Maisha hayangekuwa sawasawa. Maji ni uhai na bila maji, maisha yangekuwa sege mnege. Maisha hayangekuwa sawasawa. Kama Waswahili wanavyosema, kama Seneti na Kamati ya Mazingira haingerekebisha mambo haya, mambo haya yangekuwa goji kirba, kirba goji, yaani tunakwenda na tunarudi hapo hapo."
}