GET /api/v0.1/hansard/entries/680020/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 680020,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/680020/?format=api",
    "text_counter": 49,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 101,
        "legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
        "slug": "danson-mwazo"
    },
    "content": "Bw. Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii ili niunge mkono Hoja hii. Kabla sijazungumzia Hoja hii, leo nina huzuni sana kwa sababu tumeitwa hapa ili tuzungumzie mada hii ili tusaidie kaunti zetu zipate pesa za kufanya maendeleo na kujenga uchumi. Lakini leo asubuhi tulipata ujumbe kwamba Maseneta wa Coalition for Reforms and Democracy (CORD) wasije hapa kwa sababu uongozi wa Seneti haukukubaliana kuwe na kikao siku ya leo. Kwa niaba yangu na ya watu wa Taita- Taveta, niliamua kuja hapa kwa sababu katika Kipengele 96 cha Katiba, kazi kubwa ya Seneti ni kutetea serikali za ugatuzi na ugatuzi wenyewe. Kwa hiyo, nimekuja hapa kutetea Kaunti yangu ya Taita-Taveta. Tunapozungumza sasa, wafanya kazi wa Kaunti ya Taita-Taveta wameandikiwa barua na serikali ya kaunti kwamba hawatalipwa mishahara ya mwezi wa Julai mpaka tarehe 25. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}