GET /api/v0.1/hansard/entries/680022/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 680022,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/680022/?format=api",
    "text_counter": 51,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kama hatutapitisha Hoja hii leo, inawezekana kwamba katika mwezi wa Agosti hawatapata mshahara wao. Nimekuja hapa kuunga mkono Hoja hii kwa sababu lazima tutunze na tukuze ugatuzi. Hata kama kuna shida ya kutosikizana katika hali ya uongozi, tugekuja hapa tulumbane kwa maneno na tusikizane ili tupitishe Hoja hii. Bw. Spika, ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu pesa zitatumika vizuri. Kuna kaunti zingine ambazo zinatumia pesa hizi vibaya. Kilicho muhimu ni tukutane kwa haraka - kama itawezekana leo - na tupige kura ili pesa zitumwe kwenye kaunti. Huu ni mwaka wa mwisho kabla uchaguzi na naomba magavana watumie pesa kwa maendeleo. Huwa nawaambia wananchi kila wakati kwamba kuna sababu Katiba ilibadilishwa mwaka wa 2010. Katiba ilibadilishwa kwa sababu Wakenya walikuwa wamelalamika kwamba hakukuwa na maendeleo katika pembe zote za nchi. Hivyo, Wakenya wakaamua kuwe na ugatuzi ili kila kaunti iwe na serikali yake. Lakini, serikali si kufuja pesa ila ni maendeleo mashinani. Kwa hivyo, tusiharibu ugatuzi kwa sababu ya ufisadi. Ugatuzi uliletwa kwa sababu kila sehemu ya Kenya lazima ipate maendeleo. Kaunti ya Taita Taveta haikuwa imepata zaidi ya Kshs1 bilioni kwa mwaka mmoja kwa miaka hamsini zilizopita. Lakini tangu tuwe na ugatuzi, kila mwaka tunapata zaidi ya Kshs3.5 bilioni. Hizi ni pesa ambazo hatujawahi kupata kutoka mwaka wa 1963 hadi mwaka wa 2013. Hii ni karibu miaka 50. Bw. Spika, ombi langu ni kwamba, pesa hizi zikifika, zitumiwe kulipa mishahara kama asilimia 25 na 75 zitumike kwa maendeleo. Tukifanya hivyo, lengo la ugatuzi litatimia; na Wakenya wote wataunga mkono ugatuzi. Lakini, kwa sasa, kuna shida. Seneta akiwa katika kaunti yake, analinganishwa na mwakilishi wa eneo la Bunge, gavana na hata na mwakilishi wa wadi. Sababu ni kwamba, gavana, mwakilishi wa wadi na mwakilishi wa eneo la bunge akienda kutembelea wananchi, huwa wanapeana cheki. Sisi tukiitwa hata kwa mazishi, huwa tunakaribishwa ili washuhudie tulichonacho. Ukweli ni kwamba, mshahara ninayopata haitoshi nifanyie maendeleo. Kwa hivyo, tunaomba kwamba Seneta lazima apewe pesa za kufanya kazi ya usimamizi. Usimamizi si kutumia pesa ya maendeleo ila kama Seneta, nipate nafasi ya kuzungumza na wananchi na tufanye social audit . Wananchi wenyewe waende kukaguwa miradi ambayo pesa zao zinatumika. Wakiambiwa shule fulani imejengwa na kiasi fulani cha pesa, wataamua kama ni ukweli au la. Lakini kwa sasa, hatuna uwezo huo. Siwezi nikaenda na kutumia mshahara wangu na kufanya kazi nayo. Itakuwa vizuri kama Bunge la kitaifa litatoa pesa ili tufanye kazi zetu na tuelimishe wananchi ili wajue kazi ya Seneta ni nini. Bila kuelemisha Wakenya, wale watakaogombea nafasi za useneta mwaka ujao, itakuwa ngumu kwa sababu tutaulizwa yale tumefanya. Bw. Spika, ni kama kupanda mti na kutingiza ili matunda yaanguke halafu wengine wanakula na mimi ndiye nilipanda mti. Kwa hivyo, tutaumia na ni vizuri kama mwaka huu - hata kama hatutapata pesa - tueleze wananchi ili wajue kazi ya Seneta ni nini. Lazima wajue kwamba kazi zetu ni kutetea kaunti na kuangalia kwamba pesa zinazopewa kaunti zimetumiwa vizuri. Pesa hizo zikitumiwa vibaya, tuwe na uwezo wa kuwashtaki wanaotumia pesa za wananchi vibaya. Kwa sasa hatuna uwezo huo. Pia hatuna wafanyikazi na watu wa kutuwezesha kukagua miradi ila tunaletewa malalamishi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}