GET /api/v0.1/hansard/entries/680025/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 680025,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/680025/?format=api",
    "text_counter": 54,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kuwakabidhi pesa ili walipe wafanyikazi mishahara. Tunavyozungummza hivi sasa, tatizo ni kwamba wasipolipwa mshahara wa mwezi wa saba, watagoma. Mgomo utaathiri sekta za afya, maji na kuleta shida zingine. Bw. Spika, ugatuzi ni lazima ulindwe. Mwaka wa 1966, ugatuzi haukufaulu kwa sababu wananchi waliambiwa kwamba maseneta hawana kazi ya kufanya. Vile vile tumesikia watu wameanza kuimba tena. Wengi wamesema Bunge la Seneti linaweza kuvunjwa na Bunge la Taifa linaweza kufanya kazi ya maseneta. Ukweli ni kwamba, kama hakuna Bunge la Seneti, hakutakuwa na ugatuzi. Ni lazima tushikilie ugatuzi na tuwaambie Wakenya kwamba kila kitu kikianzishwa, huwa na shida zake. Hili ni Bunge la Seneti la kwanza kwa Katiba mpya. Limekuwa na changamoto mengi. Kwanza, ni chnagamoto la utekelezaji na la pili ni kutosikilizana na wenzetu wa Bunge la Taifa. Tatu, wananchi wa Kenya hawajazoea kupiga kura, kama hatuna pesa za kuwapa. Ni vizuri waelezwe mambo hayo kabla uchaguzi kuu lijalo. Laizma waelewe kwamba Seneta ana kazi ya kushughulikia pesa ziletwe kaunti. Kwa hivyo, hana nafasi ya kutembelea kila sehemu ya kaunti kuangalia kama pesa zimetumika vizuri. Bw. Spika, naomba wale Seneta ambao hawako hapa leo, waje haraka ili tupitishe Hoja hili. Kipenge 96 la Katiba linatupa uwezo wa kulinda na kutetea kaunti zetu. Tukipitisha Hoja hili, pesa zitakuwa serikali za kaunti. Asante."
}