GET /api/v0.1/hansard/entries/680592/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 680592,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/680592/?format=api",
"text_counter": 472,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": "Shukrani Mhe. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti iliyo mbele. Imechangiwa na Kamati ya Pamoja na Uwiano wakiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mwenyekiti wangu katika Kamati. Ninampongeza. Ni muhimu kuzingatia kwamba, katika Kipengele cha 97, wamezungumzia maswala ya jinsi ya kufurusha watu ambao wamekaa kwa ardhi isiyo yao kihalali. Hili limekuwa swala nyeti sana katika nchi ya Kenya tukizingatia matukio ya mara kwa mara ambapo tumeona wananchi wakifurushwa katika sehemu tofauti tofauti Kenya. Tumeshuhudia dhuluma ambayo wananchi wanapitia wakati wanafurushwa kutoka kwa ardhi. Mara kwa mara, wanaomiliki ardhi hii huambiwa kuwa si yao. Mara nyingi, utapata hii ni ardhi ya babu zao ambayo imenyakuliwa na mabwenyenye. Kwa hivyo, wakati tunaweka mikakati kuhusu jinsi watu watakavyofurushwa katika ardhi, liwe swala nyeti ili kufurushwa kwao kusiwe na dhuluma na kupoteza maisha yao."
}