GET /api/v0.1/hansard/entries/680808/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 680808,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/680808/?format=api",
"text_counter": 138,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Asante, Mhe. Spika. Ninaomba nitoe maoni yangu kuhusu Hoja hii ya mchezo wa kamari. Ni mchezo ambao umezua hisia mseto kwa wananchi wa Kenya hasa ikibainika waziwazi kuwa watu wengi wamepoteza fedha kupitia mchezo huu. Nchi hii ilihalalisha mchezo wa kamari kitambo kwa madhumuni ya kusaidia shughuli kadhaa wa kadhaa za nchi na hasa wale ambao hawana nafasi nzuri ya kujiendeleza aidha kimasomo, kikazi au kibiashara. Baada ya muda, imebainika waziwazi kuwa mchezo huu umechukua mwelekeo mpya na umekuwa tatizo kwa familia nyingi kwa sababu umekuwa sasa ni uraibu. Watu wamefungwa vifungo vya ajabu na mchezo huu kwa sababu ya uraibu na kuwa wasipoucheza, wako tayari kuiba na kunyanganya familia zao pesa. Wanafunzi wakipewa karo, hawalipi bali wanaingiza katika mchezo huu na mara nyingi wanazipoteza fedha hizo. Hata katika familia, watu wamejitia vitanzi, Mhe. Midiwo na Mhe. Chepkongāa wamesimulia juu ya kijana ambaye alikuwa na uzoefu wa kucheza kamari na baada ya kupoteza shilingi 80,000, aliona njia rahisi ni kujiweka kitanzi. Hapo tumempoteza kijana na fedha. Imekuwa kero kwa nchi tukizingatia kuwa nia hasa hapo awali ya kuhalalisha mchezo huu ilikuwa nzuri. Kuanzishwa kwa shughuli za mtandao kumefanya kila mtu aliye na simu ya rununu kuwa na uhuru wa kucheza kamari bila kulipa chochote. Mara nyingi tunaona vijana wetu wakijibana nyumbani na kujifungia katika vyumba vyao na hauwezi kujua wanachofanya. Mara nyingi, wanacheza mchezo huu wa kamari na hawashughuliki na masomo au kulipa karo. Nyumba nyingi zimevunjika na watu wengi wameshindwa na majukumu yao. Mhe. Midiwo alisema kuwa kuna Wabunge wa zamani ambao sasa wamekuwa maskini kwa sababu ya mchezo huu wa kamari. Tunaomba Bunge lije na sheria ambazo zinafunga njia hizi zote. Benki zetu zina sheria ya kutunza fedha za watu, kufanya malipo na kupokea fedha. Wenye michezo hii hawajulikani. Fedha zinazotumika hazina hesabu. Hakuna mtu anayeweza kukuambia wanaoshughulika na huu mchezo, mwezi huu au mwaka huu, wamepata fedha kiasi gani na wamelipa kodi kiasi gani. Faida iliyosalia wamefadhili shughuli kadha wa kadha na hamna stakabadhi zozote zinazoonyesha vile fedha hizi zimetumiwa. Mradi tu, wanapopata pesa wanazitumia vile wapendavyo. La kustaajabisha ni kuwa juzi, Sportpesa wamepeana shilingi billioni sita kwa klabu moja ya mpira Uingereza. Hatujui hizi fedha zitafuata sheria gani kutolewa nje. Je, zitafuata sheria ya nchi ama zishapeanwa? Maswali ya kujiuliza ni mengi. Je, Benki Kuu ya Kenya inahusika wakati fedha hizi zinatolewa nje, ama zinatolewa kiholela?"
}