GET /api/v0.1/hansard/entries/680812/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 680812,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/680812/?format=api",
"text_counter": 142,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kanini Kega",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1813,
"legal_name": "James Mathenge Kanini Kega",
"slug": "james-mathenge-kanini-kega"
},
"content": "Asante, Mhe. Spika kwa kunipa nafasi kuchangia Hoja hii ya Mhe. Midiwo. Kwa hisani yako, ningependa kutoa risala za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa aliyekuwa Mheshimiwa wa Nakuru Mjini, Mhe. Mark Mwithaga, aliyeaga dunia. Ningependa kufariji familia yake na ninaaomba Mungu awafariji. Hoja hii iliyoletwa na Mhe. Jakoyo Midiwo ni ya maana sana. Ukipekua magazeti matatu ya kitaifa leo, katika kurasa tano za mwisho, utapata yanawaelezea Wakenya vile watavyokuwa matajiri siku moja na kutoka kwa ufukara. Nimeangalia mambo haya na nimeona kuwa tumepoteza mwelekeo. Mataifa yanastawi kwa sababu watu wanafanya kazi. Tukiambia wananchi kwamba kuna utajiri bila kufanya kazi, tutakuwa tunaharibu nchi hii. Mhe. Spika nimesikia kuwa mchezo huu unaitwa kamari, karata na wengine wanauita bahati na sibu. Kwa hivyo, ni kubahatisha. Hakuna mambo ya kubahatisha katika maisha haya. Hili ni janga la kitaifa maanake wanaohusika katika mchezo huu ni watu ambao hawaelewi. Wanafunzi walio na simu za rununu wanashiriki katika kamari. Katika mataifa ambayo yameendelea na kunawiri, wanaoshiriki katika mchezo huu ni watu wa mapato ya kati na juu. Lakini, ukiangalia katika taifa letu, watu wanaoshiriki kamari ni watu wa mapato ya chini. Utakuta ni kina mama mboga na vijana wanaondesha boda boda . Ninaomba tuweke sheria ambazo zitatoa mwongozo katika biashara hii, ambazo hatuna. Vijana na watu wetu wametaabika. Walioongea mbele yangu wamesema kuwa kuna watu wengi ambao wameshiriki katika kamari na kupoteza fedha nyingi. Wengine wamejitia vitanzi na familia nyingi zimevunjika."
}