GET /api/v0.1/hansard/entries/681755/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 681755,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/681755/?format=api",
    "text_counter": 529,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Mswada huu ulioletwa na Mhe. Duale. Kama wanenaji wa kwanza walivyosema, ni kweli kuna ufisadi katika nchi yetu. Watu wanachukua pesa za umma na kufanya mambo ya kuwafaidi wenyewe. Utakuta mtu ameajiriwa leo na kesho amenunua nyumba kubwa ama gari la kifahari. Mswada huu utatusaidia kurekebisha baadhi ya mambo kama haya katika nchi yetu. Wawekezaji katika nchi yetu hawana imani na Wakenya kwa sababu wanapoleta pesa zao na kuwachagua watu wa kusimamia, watu wetu wanachukua hizo pesa na kuzitumia kujinufaisha. Tukiwa na sheria kama hii, nchi yetu itaendelea mbele. Katika Idara ya Polisi, haswa polisi katika bararaba zetu, wanachukua pesa kutoka kwa wananchi. Mtu akiwa hajabeba leseni, anaitishwa pesa na polisi ili awachiliwe. Tena, watu wakipelekwa mahakamani, wanahongana ili wawachiliwe. Vile Mhe. Ferdinand alivyosema hapo awali ni kweli. Katika Kaunti yangu ya Trans Nzoia, utapata afisa wa polisi akichukua pesa za umma na kununua jumba la kifahari ambalo hata mimi kama Mheshimiwa siwezi kununua. Ni kweli watu wengi wanafuja pesa katika nchi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}