GET /api/v0.1/hansard/entries/682090/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 682090,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/682090/?format=api",
"text_counter": 284,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii kuchangia Mswada wa kusitisha hongo. Tunapopitisha sheria hapa Bungeni, tunaomba kuwa viungo vya Serikali vinavyohusika vitahakikisha kuwa sheria hizi zinafuatwa. Serikali inafaa kufanya kazi yake hususan vitengo vya polisi na usalama na kile kinachokabiliana na ufisadi kuhakikisha kuwa sheria hizi zinafuatwa. Sheria hizi zikifuatwa, ufisadi utaisha. Mwananchi wa kawaida hawezi pata huduma za afya, ambazo ni haki yake, ilhali analipa ushuru. Kule hospitalini, inabidi mtu atoe hongo ili aweze kuona daktari. Ni jambo la kusikitisha sana. Tatizo haliko hapo peke yake lakini liko katika sehemu tofauti tofauti mpaka barabarani kuhusu polisi. Wananchi walioamua kuingia katika sekta ya usafiri wanapata shida sana. Wanalazimishwa kutoa hongo na polisi na wakati mwingine wanasingiziwe makosa ambayo si ya ukweli. Hili ni jambo ambalo linaozesha nchi yetu. Nchi ya Kenya inaweza kuwa kati ya zile nchi ambazo zimeendelea sana. Mwenyezi Mungu ametubariki na amani na Wakenya wengi wenye akili za kukuza uchumi. Uozo wetu mkubwa wenye kutudhuru zaidi ni ufisadi. Kandarasi katika Serikali Kuu na serikali za kaunti hazipeanwi inavyotakikana kisheria. Ni mpaka watu watoe hongo ndio kandarasi zao ziangaliwe na wakubali kugawanya senti na maafisa wa Serikali. Mhe. Naibu Spika wa Muda, utashangaa kuwa ni shida kwa wananchi kupata vitambulisho. Mtu akifika pale, kitambulisho hakipatikani lakini akitoa shilingi elfu moja, kwa mfano, kitambulisho chake kinapatikana. Saa hii, Wakenya wengi bado hawajasajiliwa kuwa wapiga kura. Tunataka Wakenya wengi wasajiliwe kupiga kura. Uozo huu unatoka juu kwenye viongozi mpaka kwa wafanyikazi wa chini katika nyanja za Serikali. Ningetaka kuilaumu Serikali zaidi kuliko sekta za kibinafsi kwa sababu sekta ya kibinafsi ni lazima ipitie kwa Serikali ili ifanye kazi zake. Maswala ya hongo yanawasumbua wananchi sana kwa sababu utaona kuna kampuni ambazo zinachukua ardhi ya wananchi kiharamu. Kule Kwale ninakotoka, kuna shule moja katika Wadi ya Kasemeni ambayo ardhi yake inataka kuchukuliwa na kampuni fulani. Mara nyingi utaona ufisadi umeingia mahali kama hapo na sheria haikufuata mkondo wake vizuri."
}