GET /api/v0.1/hansard/entries/682092/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 682092,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/682092/?format=api",
"text_counter": 286,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Pia, katika sekta ya siasa, utaona kuwa wananchi wamezoea kupewa hongo katika maswala ya kuwachagua viongozi. Jambo hili limewafanya Wakenya kuenda njia mbaya kwa sababu mara nyingi, wananchi huenda wakamchagua mtu atakayewapatia pesa zaidi, atakayewanunulia nguo au chakula ili wamukubali kama kiongozi. Mara nyingi, mtu atatumia pesa nyingi na akiingia katika uongozi atatafuta njia za kuregesha zile pesa zake. Kando na kuwachagua viongozi wabaya kwa sababu ya hongo, kuna shida ya kuwa wananchi wetu, kwa sababu ya kutegemea sana kupewa hongo na wanasiasa, wanapunguza nafasi yao ya kujibunia njia tofauti tofauti za kujiimarisha kisiasa. Mara nyingi utamsikia mtu ako na shida fulani na njia pekee ambayo ataweza kupata msaada ni kupitia kwa mwanasiasa badala ya yeye mwenyewe kubuni suluhisho. Hii inatokea kwa kuzoea pesa. Hii ni mila ambayo imekuwa kwa nchi yetu kwa miaka mingi na itachukua muda kuiondoa. Kama nilivyozungumza awali, vitengo vya usalama kama polisi na shirika la kupigana na ufisadi wakichukulia kazi yao kama inavyotakikana, haya mambo yataisha nchini yetu na tutasonga mbele. Kwa hayo machache, shukrani kwa kunipa muda huu wa kuchangia."
}