GET /api/v0.1/hansard/entries/682936/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 682936,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/682936/?format=api",
    "text_counter": 142,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Aburi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2901,
        "legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
        "slug": "lawrence-mpuru-aburi"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninaunga mkono Mswada huu na ninasema asante kwa ndugu yangu mpendwa kwa kunipatia muda wa dakika moja nichangie kidogo. Serikali ya Rais Uhuru Muigai Kenyatta imepeleka mashini katika hospitali nyingi katika kaunti. Imetoka katika Serikali ya Kitaifa na kwenda katika serikali za kaunti. Imekuwa vigumu kwa magavana kuwasaidia madaktari kupandishwa vyeo. Kwa mfano, katika Kaunti ya Meru, mashini za mabilioni ya pesa zilipelekwa huko lakini sasa hivi zimefungiwa katika stoo. Hazitumiki kwa sababu gavana alikuwa anataka kuweka saini makubaliano kwamba yeye ndiye anayeshughulika na mashini hizo. Kama si hivyo anataka Serikali ya Kitaifa ipeleke mashini hiyo. Hii Ndio maana tunasema kama inawezekana sekta ya afya inafaa irudi kwa Serikali ya kitaifa na itoke kwa serikali za kaunti kwa sababu wagonjwa hawana vitanda katika hospitali nyingi wakati huu. Wagonjwa watatu wanalala kwa kitanda kimoja. Mwananchi wa kawaida ana shida. Wanaofurahia ni wale ambao wana pesa za kwenda katika hospitali za kibinafsi. Baadhi ya madaktari wana hospitali huko nje. Kama unafanya kazi ya Serikali, fanya hiyo kazi ya Serikali. Hufai kuwa na hospitali mbili."
}