GET /api/v0.1/hansard/entries/683580/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 683580,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/683580/?format=api",
"text_counter": 280,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nassir",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "kutoa wasia kwa mabenki ili tuwasaidie vijana kwa kuwapatia mikopo waweze kuweka akiba zao pamoja na mambo ya kujenga masoko. Ripoti hii inaonyesha wazi kwamba Kshs180,000,000 zimepotea kiholela. Kamati hii ilidadisi mashahidi 19 kwa muda unaohitajika. Ni ombi letu kwamba Serikali iwachukulie hatua mwafaka wahusika wote kwenye sakata hii. Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa YEDF waliketi chini wakaamua kuchukua Kshs400 milioni kutoka kwa YEDF na kuziweka katika Chase Bank ili pesa hizo ziweze kuzaa riba badala ya kutumika kuwasaidia vijana wetu. Fedha hizo ziliibiwa taratibu tarehe mbalimbali, zikiwemo tarehe 11 Februari 2015, ambapo Kshs115,710,000 ziliibiwa, na tarehe 27 Aprili 2015, kiasi cha Kshs65,84,946 kiliibiwa. Jambo la kushangaza ni kwamba Mwenyekiti wa Bodi ya YEDF aliandika barua kwa benki na kuishauri kwamba mtu mmoja pekee ndiye aliyeruhusiwa kuweka sahihi kuhusu hizo Kshs400 milioni. Jambo hili ni la kihistoria nchini Kenya. Haijawahi kutokea mtu mmoja akawa ni mwenye kupatiwa ruhusa ya kuweka sahihi peke yake anapotoa fedha za umma kutoka benki. Hata Waziri katika Hazina ya Taifa hana ruhusa ya kufanya jambo kama hilo. Hali hiyo ilisababisha pesa hizo kutolewa kutoka benki hiyo na kuhamishwa kwenye shirika ambalo halikufanyiwa ukaguzi wa aina yoyote kubaini iwapo linafaa kutoa huduma za tehama. Kwa ruhusa yako, Mhe. Naibu Spika wa Muda, nataka kuwafahamisha Wabunge wenzangu kwamba “tehama” kwa lugha ya Kiingereza ni “ Information and CommunicationTechnology (ICT)”. Baada ya hapo, shirika hilo likawa na hakikisho tayari na kuagiza shirika la YEDF kulipa shirika moja mamilioni ya pesa. Waziri mwenye kuhusika na shirika hili alikuja kwa Kamati na akatoa ushahidi kwamba katika mwaka wa 2013, shirika hili liliweza kuweka mkataba na likawa na uhusiano na kampuni fulani na wakalipwa Kshs5.5 millioni peke yake."
}