GET /api/v0.1/hansard/entries/683582/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 683582,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/683582/?format=api",
"text_counter": 282,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nassir",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Nikimalizia, Ripoti hii inaonyesha wazi vile pesa zilitumika. Tunaisihi Serikali ifanye inavyohitajika na mojawapo ni kushika zile raslimali. Katika Ripoti hii, tumefanyia Serikali udadisi na uchunguzi. Wabunge 27 and makarani sita, tulihakikisha kwamba njia ambayo zile fedha zilitumika imejulikana. Majumba ya kifari yalinunuliwa katika mji huu wa Nairobi. Pesa zilivyoenda kwa wenye kuhusika na hongo zilitolewa na kutumika. Ni ombi letu kwamba Wakenya wahakikishe Serikali imefanya jukumu lake na tatizo la nchi limeishia kuwa si wizi tena. Tatizo ni kuwa watu wanaiba jinsi ya wezi wa mabavu bila kujali jambo lolote. Mtu anahisi kuwa akiweka sahihi na kutoa mamilioni kama yale, ataishi na hakuna jambo ambalo litafanyika. Ikiwa Serikali ina nia ya kuendesha maswala ya vijana, basi ni lazima hatua iweze kuchukuliwa kwa kila jambazi aliyeiba pesa hizi."
}