GET /api/v0.1/hansard/entries/68383/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 68383,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/68383/?format=api",
"text_counter": 246,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Joho",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 30,
"legal_name": "Hassan Ali Joho",
"slug": "hassan-joho"
},
"content": "Jambo la nidhamu,Bw. Naibu wa Spika. Jana, nilipokuwa nikitazama runinga, nilimwona Kamishna wa Polisi akieleza kwamba uteguaji wa mabomu siku hizi umekuwa ukitendwa na watu waliojiunga na uislamu hivi karibuni. Ninaona mambo mawili. Kwanza, hakuna uwezekano kwamba uchunguzi wa kisa cha basi la kampuni la Kampala Coach ungefanywa siku hiyo na kukamilika siku hiyo ndipo isemekane ni fulani. Je, ni haki kwa Waziri kusema kwamba hawahusishi sana waislamu na ugaidi na hali Kamishna wa Polisi amesema wazi kwamba ni Waislamu wapya wanaotekeleza mashambulizi ya mabomu?"
}