GET /api/v0.1/hansard/entries/685764/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 685764,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/685764/?format=api",
    "text_counter": 397,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Mumo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 808,
        "legal_name": "Rose Museo Mumo",
        "slug": "rose-museo-mumo"
    },
    "content": "Ahsante Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Nachukua nafasi hii kuwapa hongera wanariadha wetu ambao walikuwa Rio. Tunasema ni ahsante kwa walivyofanya. Kweli, wametufanya kuwa na furaha kubwa. Ningependa pia kumrudishia shukrani mwanariadha Rudisha ambaye aliweza kufanya jambo la kipekee ambalo tulilifurahia sana kama Wakenya. Kwa wote walioweza kushiriki, pongezi. Sisi kama viongozi, hatukupenda mambo ya ufisadi yalioendelea na kuwatesa watoto walioenda kule Rio."
}