GET /api/v0.1/hansard/entries/688536/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 688536,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/688536/?format=api",
"text_counter": 77,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu Spika. Ningependa kuomboleza na familia ya Mzee Dennis Akumu, kiongozi aliyeheshimika humu nchini. Alijihusisha na vyama vya wafanyikazi na kuvuma sana Afrika nzima. Ningependa kuwasihi Wabunge wenzangu tumpe heshima itakayofanya akumbukwe milele. Kama wanasiasa wachanga, ni muhimu tukumbuke kuwa Mzee Akumu alipigania haki za wafanyikazi nchini Kenya na atakumbukwa milele. Kwa wale ambao hawajui, Mzee Akumu alifanya kazi na babangu aliyekuwa Mbunge na Waziri katika Serikali ya Rais Jomo Kenyatta. Namshukuru Mbunge wa Nyakach kwa kuleta mazungumzo haya na kumpa rambirambi zetu kama Bunge la Kitaifa. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi."
}