GET /api/v0.1/hansard/entries/68956/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 68956,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/68956/?format=api",
    "text_counter": 387,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Bw. Spika, ninasimama kupinga Hoja hii kuhusu kwenda likizo. Itakumbukwa kwamba Bunge hili hapo awali lilipitisha Hoja nyingine ambazo baadaye zilikuwa majuto. Majuto baadaye huwa mjukuu. Tunahitaji nafasi ya kutosha kutafakari na kuchambua Hoja muhimu kama hii inayohusu utekelezaji wa Katiba. Kwa hivyo, saa ambazo sisi Wabunge tutapewa kuichambua ni chache sana. Itakumbukwa tena Wabunge wanapoketi kuzungumzia Hoja kwa zaidi ya masaa manne, wengi wao hupatwa na lepe la usingizi. Wengine wetu hapa umri umewapa kisogo na hawatashughulika na mambo muhimu. Kwa hivyo, ninapinga Hoja hii."
}