GET /api/v0.1/hansard/entries/689950/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 689950,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/689950/?format=api",
"text_counter": 85,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Ahsante. Mhe. Spika. Nami nimesimama kuiunga mkono Hoja hii kwa maana kikao cha Kamati inayohusika na Shughuli za Bunge jana kilijadili utaratibu utakaofuatwa na kuamua kwamba litakuwa jambo la busara tuwe na kikao kesho asubuhi ili tupate nafasi ya kuishughulikia Miswada muhimu ambayo iko mbele yetu, na ambayo tunahitajika tuikamilishe kabla hatujaanza likizo ambayo inatarajiwa kuanza Ijumaa. Kwa hivyo, tunawaomba Waheshimiwa mkubali ombi hili ili tupate kumaliza shughuli hizi. Naliunga mkono ombi hili, Mheshimiwa Spika."
}