GET /api/v0.1/hansard/entries/690620/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 690620,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/690620/?format=api",
    "text_counter": 208,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "Nimeshukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Hii itakuwa sheria ya kufana sana, tukizingatia makosa yanayofanywa na wapiga kura na baadhi ya wagombeaji viti vya uchaguzi. Imebainika kwamba akina dada mara nyingi huwa wanazuiwa kugombea ama kushiriki kwenye chaguzi huru kwa sababu ya makuruhu na dhuluma wanayofanyiwa na baadhi ya wapinzani wao wa kiume. Kifungu cha 16 kinazungumzia ubebaji wa wapiga kura kutoka sehemu moja hadi nyingine na kuwaregesha. Hili limekuwa pigo kubwa sana kwa akina dada wanaogombea viti. Wakati wa kuwasajili wapiga kura, wapinzani wengine huwasafirisha wapiga kura kutoka wilaya moja hadi nyingini. Kifungu cha 18 kinaangazia suala la baadhi ya waajiri ambao huwazuia waajiriwa wao kwenda kupiga kura. Ninavyoelewa ni kwamba kuna kampuni ambazo zimeajiri zaidi ya Wakenya 600 ama 1,000. Wakenya hao wamekatazwa kuweka vituo vya kupigia kura miongoni mwao. Siku ya kupiga kura, wenye kampuni hizo huwazuia wafanyikazi wao kutoka nje ili kwenda kupiga kura. Huo ni unyanyasaji na ukiukaji wa sheria za Kenya. Mengi yamesemwa kuhusu sheria za upigaji kura. Ninataka tu kuchangia kuhusu maneno ya kugura vyama vya kisiasa. Kuwakataza wagombeaji kuhama vyama vyao vya kisiasa baada ya uchaguzi wa mchujo ni kuturegesha katika hali ya chama moja. Sisi sote katika Bunge hili tunajiunga na vyama vya kisiasa kwa sababu ya kuamini miundo misingi ya vyama hivyo. Litakuwa jambo la kufana iwapo tutaamini miundo misingi ya vyama hivi na tukae katika vyama na tutafute namna ya kusuluhisha matatizo yote ambayo yatatokea baada ya chaguzi za mchujo. Iwapo mtu anahisi kwamba ana nguvu za kuunda chama chake, agure vyama vya kisiasa kabla ya uchaguzi wa mchujo. Katika Bunge hili, mimi ni mmoja wa watetezi wa haki za kibinadamu na ukiukaji wa haki za kibinadamu. Mhe. Spika wa Muda, sheria hii imezungumzia, haswa usawa wa kijinsia, baadhi ya wagombeaji na wapiga kura. Ninapoongea kuhusu usawa wa kijinsia, tumeongea sana kuhusu uteketaji wa wasichana. Litakuwa ni jambo la maana kutunga sheria ambayo inaidhinisha na kulazimisha kutahiri kwa wanaume, katika nchi hii yetu ya Kenya. Mbali na kudhibiti makali ya ugonjwa wa ukimwi, imebainika kwamba iko pia na faida ya kusaidia kukomaa, ili tusione wanaume wazima wakiketi kwa barabara kulazimisha Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ing’atuke. Tunajua kuna sheria ambayo imetungwa ambayo inasema wazi kuhusu kung’atua Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka."
}