GET /api/v0.1/hansard/entries/690645/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 690645,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/690645/?format=api",
    "text_counter": 233,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, ningependa kutoa shukrani kwa wakati huu ambao nimepewa kuunga mkono Mswada huu. Ni maoni yangu kuwa pale ambapo kuna vipengele ambavyo vinahitaji marekebisho, vifanyiwe marekebisho ili angalau tupate sheria ambazo zitadumu. Wakati umefika kwa sisi kuangalia kuwa wakati wa uchaguzi, wale ambao wanafanya dhambi wakati wa uchaguzi nao pia waadhibiwe vilivyo. Ningependa kuunga Mhe. Millie Odhiambo mkono kuwa lazima tuhakikishe tunapofanya mchujo, atakayepewa tiketi ya chama akifanya makosa lazima ahusishwe katika dhuluma ambazo zimetajwa na vipengle hivi ili aadhibiwe kwa mujibu wa sheria."
}