GET /api/v0.1/hansard/entries/690881/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 690881,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/690881/?format=api",
    "text_counter": 202,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nakara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2926,
        "legal_name": "John Lodepe Nakara",
        "slug": "john-lodepe-nakara"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi ya kuchangia mjadala huu kuhusu Hoja hii muhimu. Kwanza, nakushukuru wewe na kikao chako cha maspika kwa jinsi ulivyoonyesha uongozi katika Bunge hili, kama tu ulivyochangia jambo la Mhe. Nyikal. Uko na hekima. Mambo yako ni machache lakini uko na hekima na unajua sheria. Pili, nawashukuru watu wa Eneo Bunge la Turkana ya Kati kwa kunichagua kuwa Mbunge wao. Nimejifunza mambo mengi tangu nilipokuja katika Bunge hili. Nimewakuta wazee wenye hekima na nimejifunza kuwa mvumilivu. Pia, nimejifunza jinsi ya kujadili mambo yanayowaathiri watu wangu. Ningependa pia kuwashukuru Wabunge kwani tumefanya kazi pamoja. Licha ya kuwa na mgawanyiko katika hali ya vyama, tumedumisha heshima. Tumeheshimiana bila kujali vyama ama kabila. Ningependa pia kukushukuru kwa sababu ya sheria ya riba ambayo tulipitisha katika Bunge hili. Wananchi kule nje wanashukuru sana kwa sababu benki nyingi zilikuwa zikitoza riba za juu na wananchi walikuwa wakiumia na kulalamika kwa sababu ya kulipa riba za juu. Rais alipoweka sahihi katika Mswada huo na ukawa sheria, Kenya nzima ilishangilia na hiyo yote ilikuwa kazi ya Wabunge ambao wako mahali hapa. Nashukuru kwa nafasi hii ya kwenda likizoni ili tupate nafasi ya kutangamana na watu wetu na pia kuwaelimisha kuhusu sheria ambazo tumetunga hapa ili wajue na wasitumbukie katika mtego wa sheria. Hiyo ni kazi yetu kama Wabunge. Tukienda kule kutangamana na hawa, tutawaeleza kuwa tumepitisha hii. Mheshimiwa Spika ni nafasi ya kwenda kuwa na watu wetu kujadili juu ya miradi ambayo tunataka ihifadhiwe mwaka huu. Tujue kutoka kwa hao na tusikie miradi ambayo wanahitaji ili tutakapokuja mahali hapa, kupitia Fedha za Eneo Bunge tuone ya kuwa miradi ambayo wananchi wametaka The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}