GET /api/v0.1/hansard/entries/690882/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 690882,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/690882/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nakara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2926,
        "legal_name": "John Lodepe Nakara",
        "slug": "john-lodepe-nakara"
    },
    "content": "imetimika na imetendeka kama vile wananchi walivyokusudia. Mheshimiwa Spika ningependa kukushukuru kwa sababu ni wakati mwingine ambao tungependa kwenda kupumuzika ili tukija mahali hapa tuwe na nguvu ya kuendesha kazi. Mwisho, ningependa kuwaambia Wabunge wenzangu, tutakapokutana katika mikutano ya siasa hapa na pale tudumishe heshima na ule urafiki wetu maana wakati mwingine tukifika mahali pale unapata ya kwamba tunatupiana maneno makali na mambo ambayo si mazuri mbele ya wananchi, tunapoteza heshima ya Bunge hili. Kwa hiyvo, ninaomba tuendelee na ile heshima tuliyokuwa nayo mahali hapa. Hata kama hao ni wa kikundi ama chama kingine tukikutana tujue ya kwamba sisi ni Wabunge na tutarudi kwenye Bunge na tuendelee kuheshimiana. Hilo ndilo ambalo ningependa kuwaambia Wabunge. Ninajitayarisha kuenda kukaa na wananchi wangu. Mungu awabariki wote asanteni."
}