GET /api/v0.1/hansard/entries/690884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 690884,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/690884/?format=api",
    "text_counter": 205,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2308,
        "legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
        "slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
    },
    "content": "Shukrani Mheshimiwa Spika kwa kunipatia nafasi hii. Ningelipenda kwanza nikushukuru wewe kikamilifu kwa sababu ya vle ulivyopambana katika hali ya kudumisha na kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa. Ninakumbuka mwaka wa 1967 marehemu muanzilishi wa taifa hili, Hayati Mzee Jomo Kenyatta aliulizwa na rafiki yake Hayati Julius Nyerere: ―Ni kwa nini wewe unatembea na askari wengi?‖ naye akajibu ―Ninatembea na askari wengi kwa sababu Tanzania si kama Kenya. Kenya ina wanaume.‖ Na ninataka kukuhakikishia umepambana vikali Mheshimiwa Spika kwa sababu Bunge hili lina wanaume kuliko Mabunge yote ulimwengni. Kwa hiyvo, umefanya kazi nzuri pamoja na kamati yako na ninakuombea likizo njema ili uweze kutafuta nguvu kwa sababu wanaume wale bado wako na watakuja na wanakungoja uwaongoze kisawasawa. Mheshimiwa Spika, nataka kuunga mkono vikamilifu Mswada ambao umeletwa mbele yetu kwa sababu tumefanya kazi nzuri na Kenya nzima ikafurahia. Kenya imefurahia kupitishwa kwa Mswada wa kupunguza riba inayotozwa na benki. Wajua mimi huingia vichochoro vya Nairobi hii. Nimekunywa chai ya watu karibu 20 na nikiuliza kwa nini wananinunulia chai ilhali hawanijui, wanasema kwamba wamefurahishwa na kazi nzuri ya kupunguza riba. Kwa hivyo, hiyo ni kazi ambayo imeweza kulifanya Bunge hili lipate sifa na sifa ile yote imekuja kwa sababu ya usimamizi wako Mheshimiwa Spika. Nikirudi katika sheria za vyama, nataka niunge mkono kikamilifu kwamba watu wasiruke hapa na pale. Ni lazima kila mtu afanye kazi yake kikamilifu na kama anaunga mkono chama chake kikamilifu, basi hapo hawezi kutingishwa na mtu yeyote. Najua kwamba kuna wengi hawakusikia raha kwa sababu pengine wamepitisha Mswada huu kwa sababu baba, Rais, Mheshimiwa Wetangula au Kalonzo amependa. Wengine wao walikuwa hawapendi lakini wamefanya kwa sababu hiyo. Mimi naomba kila mtu ambaye yuko katika Bunge hili ahakikishe kwamba Mswada huu ameutilia maanani na ameufurahikia kwa sababu huwezi kubwagwa na yeyote wakati wewe unafanya kazi nzuri katika chama chako. Na mimi ninasema wale wanasema kuna mayatima, wale si mayatima. Wale wamekata shauri, wameondoka kwenye mlo na kuingia katika sehemu ambazo zina giza kidogo. Wale in mashujaa kwa sababu kuacha chakula hapa na kuenda kutafuta mahali pengine, huo ni ushujaa mkali na wanastahili sifa badala ya kuitwa mayatima."
}