GET /api/v0.1/hansard/entries/690897/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 690897,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/690897/?format=api",
"text_counter": 218,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hoja hii. Kwanza, mimi pia naungana na wenzangu kukupa pongezi nyingi sana kwa namna ambavyo umetuelekeza katika Bunge hili. Haikuwa rahisi. Kama vile ndugu yangu Mhe. Mwanyoha alivyosema, Bunge hili liko na wanaume. Vile vile naongezea sisi kule Pwani twasema liko na nyangumi na papa ambao wanaweza kutafuna mtu akifanya mchezo. Kwa hivyo, tunashukuru kuona kuwa mawimbi yale umeweza kuenda nayo na kutupeleka kwa njia ya sawasawa. Pili, nakupongeza kwa busara yako. Nimekuja ofisini kwako mara kwa mara nikitaka kufafanuliwa vipengele vya sheria na umenieleza namna ya kufanya kazi ambayo nimepewa na watu wangu katika Bunge hili. Vile vile, nimesikia wenzangu wakisema ulikuwa unalinda mayatima. Lakini kati ya wale mayatima unaowalinda, nataka kuzungumza kama Naibu Katibu Mtendaji wa chama cha Wiper Democratic Movement of Kenya - ndungu yetu Mhe. Munuve hajakuwa yatima. Yatima ni yule ambaye amefiwa na baba na mama. Baba Kalonzo bado yuko na analinda watoto wake. Mhe. Munuve ni mtoto mpotevu, sio mtoto ambaye ameachwa na baba. Ni lazima tuhakikishe sheria tunazounda zitafaa wananchi wetu ambao wametutuma hapa kuwawakilisha. Shida za Wakenya nyingi sana ni umasikini, ukosefu wa elimu na ajira. Ndio maana ikifika wakati wa uchaguzi tunaona fujo nyingi zinatokea na watu kutumiwa. Asilimia kubwa ya wananchi wetu wangelikuwa na ajira na elimu ya kutosha, hawangeliweza kupelekwa kwa njia ambayo sio sawasawa. Kwa hivyo, ni wakati wa Serikali kuweka mikakati muafaka ambayo itahakikisha kuwa watoto wetu na jamii zetu wanaweza kusoma na kuwapatia ajira kwa wingi. Nimesikia Mbunge mwenzangu akizumgumza kuhusu kufurahishwa na vile uhusiano umeimarika kati ya Turkana na Pokot na akasema kuwa atachukua fursa hii kuona kuwa wakirudi pale nyumbani watashikana ili wazungumze na wananchi wao. Sisi kule Pwani, ambapo matatizo kama haya hayajatupata sana, kama Wabunge marafiki watataka kuzungumza na ndugu zao pale, tuko tayari kujitolea pia ili kuzungumza na jamii ili sote tushikane tuonyeshane ile ishara ya udugu. Tuonyeshe kuwa tunaweza toka hapa na kuhubiri amani katika sehemu mbalimbali za nchi hii. Natoa pongezi nyingi sana kwetu kwa kupitisha ule Mswada wa riba ya mikopo ya benki. Pia, ningependa kukushukuru sana kwa sababu wakati wa kujadili Mswada huo nilipata nafasi ya kuchangia. Kabla Mswada huo kupitishwa, watu waliishi katika hali ya ate ate na maisha yakawa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}