GET /api/v0.1/hansard/entries/690923/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 690923,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/690923/?format=api",
    "text_counter": 244,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Machira",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 769,
        "legal_name": "Jane Agnes Wanjira Machira",
        "slug": "jane-agnes-wanjira-machira"
    },
    "content": "Hon. Spika, nashukuru kwa kunipatia fursa hii kuchangia mjadala wa lala salama tukielekea kwa likizo. Leo ni siku kubwa zaidi kwani tumepitisha Miswada mitatu muhimu zaidi katika Kenya yetu. Miswada hii ni muhimu zaidi kwa sababu tumekuwa na Miswada mingine mizuri lakini hatujapitisha Miswada kama hii inayohusu uchaguzi na kuhamahama vyama. Tungepoteza mwelekeo wakati sisi sote tulikuwa tumekataa, lakini kwa kuwa na uongozi mwema ambao uko katika Kenya, tukihusisha Rais wetu, naibu wake na kinara wa upande ule wa wasio wengi, tumefanya vyema. Pengine hatutajua matunda ambayo tumevuna leo lakini tunajua ya kwamba tuna matunda ambayo tutaona yakivunwa. Huu ni wakati wa kurekebesha vile vyama vimekuwa vingi zaidi na viliyvo na watu wachache zaidi. Kazi ya hivyo vyama vidogo ni kutafuta fedha na kupoteza kura na kutoonyesha Kenya kama tunaendelea kukomaa. Sasa tumechukuwa mwelekeo ambao tutaonyesha kukomaa. Leo tumepitisha Mswada ambao ni wa ushirikiano wa Wakenya na baina ya Serikali ya Uingereza. Ushirikiano huu ni wa kusaidia kustawisha usalama katika nchi hii yetu na wao. Mimi nikiwa nimetoka Laikipia tulifurahi zaidi kwa sababu ya kudumisha uhusiano huo. Sisi tumefaidika kutokana na uhusiano huo. Askari ambao wametoka Uingereza wamekuwa wakitusaidia katika mambo yetu ya kawaida kama vile kujenga barabara, kujenga viwanja na hata kuwapatia vijana wetu kazi. Vijana kutoka Laikipia wamefaidika kwa kupata kazi na tumefurahi zaidi kwa sababu ya kuidhinisha huo uhusiano. Ikiwa kuna Wabunge ambao wamesema huu uhusiano si mzuri, sisi tuna wakati wa kurekebisha. Tukisema hivyo, tunajua hapo mbeleni Kenya ililipwa ridhaa na Uingereza. Watu kutoka Samburu na Laikipia walifaidika na wamefurahi sana. Baina ya wale waliofaidika, waliondoka vijijini na kuelekea mijini kustarehe. Leo hawana chochote na bado wana maumivu yaliyolipiwa ridhaa."
}