GET /api/v0.1/hansard/entries/691125/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 691125,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/691125/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "wanavyotumia silaha zao. Wanapoenda kwa mafunzo, wanawacha silaha zao nje. Wanatupa mabomu, risasi na kila aina ya silaha. Mnajua maeneo yetu ni ya wafugaji. Ng’ombe zinatembea zikitafuta nyasi na watoto wanazichunga. Watu wengi wamepoteza maisha yao. Hilo ni jambo moja linalopaswa kuangaliwa. Jambo la pili ni hili: Tangu wakuje huko, hatujapata faida kutoka kwao kama vile msaada wa maji kwa mashule. Bado tuna shida ya maji na barabara. Hata wakitengeneza barabara, wanapitisha tinga tinga mara moja na baadaye inaonekana ni kama haikutengenezwa. Wanadanganya wananchi kwamba wataleta maji, watatengeneza barabara na kuleta hospitali, lakini bado hatujaona wakifanya kitu."
}