GET /api/v0.1/hansard/entries/691126/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 691126,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/691126/?format=api",
"text_counter": 194,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Ikiwa hii sheria itatiwa sahihi, waende watutengenezee kitu kile kitadumu wala si kuwadanganya wananchi. Wakituwekea hospitali, barabara au kisima cha maji, itasaidia kila mtu kwa sababu wanadanganya wananchi. Wakati wanalipa malipo ya wale watu wameaga, hawaangalii wale wanyama ambao wameumizwa na hayo mabomu. Wakati ng’ombe na mbuzi wanakufa kwa sababu ya hayo bomu, hawachukulii maanani. Kwa hiyvo, ningependa sheria hii iangalia vile vitu vinasaidia wananchi. Mahali pale wanafanyia mazoezi, kuna mahali ambapo walikuwa wamepewa na sasa wamesongeza mipaka had kwa mashamba ya jamii. Wakati wanaulizwa ni kwa nini wamesonga, hata hawajali mtu. Kwa sababu Mwenyekitu yuko hapa, ningependa waangalie wananchi. Waanze kuongea na mwanacnhi na viongozi wale wako pale. Watoto wetu wakati wamefunga mashule, unapata wamezingira hizo kambi zao. Wanadanganya watoto, wawe ni wasichana au vijana. Wanasema wameandika watu kazi. Ningeomba Mwenyekiti wa Kamati atoe hiyo orodha ya wale wameandikwa kazi. Hiyo ni kwa sababu unakuta msamburu ni yule ameandikwa kuosha nguo au vyombo. Hiyo si kazi. Kwa hivyo, ni muhimu tuambiwe ni kazi gani zimepeanwa ndio tupate kujua. Sana sana, wanatumia watoto wetu kuchunga kambi zao. Hiyo pia si kazi kwa sababu wanafuta watu kila dakika. Wanaandikwa leo na keshoye wanafutwa."
}