GET /api/v0.1/hansard/entries/691128/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 691128,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/691128/?format=api",
    "text_counter": 196,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Pia mahali pale wamepewa, ni muhimu waweke ua. Kwa sababau wasipofanya hivyo, inakuwa shida. Kila mtu anaingia. Watu wetu wameumia sana. Watu kadhaa wamekatwa mkono na wao hawajali. Kuna mzee mmoja wanasema haijulikani ni nini ilimkata, ilhali alikatwa na mashini yao. Kwa hivyo, tuna shida nyingi na ni muhimu iangaliwe wakati sheria hii inapitishwa. Hatutapinga njia ya sheria kupitishwa, lakini faida ya mwananchi aliye pale iangaliwe na ile njia wanatumia--- Wakipata watu watatu au wane, wanafikiri wanawakilisha hiyo jamii. Tungewaomba waongee na jamii kwa jumla. Kamati ya Ulinzi na Maswala ya Kimataifa ilitembea huko katika Bunge la Kumi. Ningeomba Mwenyekiti wa kamati ya sasa - kwa sababu ako hapa - aende achukue hiyo Ripoti ajue ni nini walizungumzia huko na ni nini waliona huko."
}