GET /api/v0.1/hansard/entries/691155/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 691155,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/691155/?format=api",
"text_counter": 223,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bedzimba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1933,
"legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
"slug": "rashid-juma-bedzimba"
},
"content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kupenyeza sauti yangu hasa katika Hoja hii ya ushirikiano baina ya Serikali yetu ya Kenya na Uingereza kupitia muungano wa majeshi. Mimi nitaunga mkono Hoja hii ikiwa taratibu fulani zitafuatwa. Kwanza, wahakikishe kuwa mahali ambako jeshi hili litakuwa likifanyia mazoezi, zile silaha zote ambazo hazikulipuka zilipuliwe ili mahali pale pawe salama. Wakenya wengi sana wamepata ulemavu kwa ajili ya silaha ambazo Waingereza walitumia na kuchimbia chini ya ardhi yetu. Nazungumza haya kwa sababu nilikua askari kwa miaka tisa. Tumetembea sehemu nyingi ambako kambi za Waingereza ziko. Mabomu mengi sana ambayo hayakulipuka bado yako ardhini. Watu wanaoishi katika sehemu hizo ni wafugaji na mara kwa mara, wanalipuliwa wakiwa katika shughuli zao za kulisha mifugo. Waingereza pamoja na serikali nyingi za ulaya zilitukoloni kabla tupate uhuru wetu. Walichukua rasilmali zetu nyingi sana. Sasa tuko huru. Tusipeane nafasi katu ya rasilmali zetu kuchukuliwa tena. Ikiwa tutakubalia waje wafanyie mazoezi katika ardhi zetu ili kwamba wazoee mazingara ya Afrika, basi ni lazima kuwepo na taratibu wa kuhakikisha kwamba mambo fulani yanatekelezwa mwanzo ili kufaidi jamii zinazoishi mahali pale. Kwanza wakija, lazima waje na bajeti ambayo itaonyesha kwamba watajenga shule za msingi, shule za sekondari na hosipitali kubwa ili wakaazi wa maeneo hayo waweze kufaidika. Silaha ambazo zinatumika zina madhara. Hakuna silaha ambayo baada ya kutumika, inakosa madhara. Kuna vitu ambavyo tunaweza kuona na vile hatuwezi kuona. Lazima wajenge hospitali kubwa na iwe na madawa ya kutosha ili watu wetu waendele kupata matibabu kama ambavyo jeshi lao hufaidika na matibabu mazuri. Ni aibu kwamba kambi ya wanajeshi wa Uingereza ina vitu vingi vinavyohusiana na jamii kuliko zile jamii zinazoishi katika haya maeneo tuliyowatengea kufanyia mazoezi ya kivita. Zile jamii maskini, kwa kukosa maji na chakula, huenda kuishi karibu na kambi hizo ili kutafuta misaada. Hii ndiyo sababu wale wanajeshi wanachukua nafasi ya kuwadhulumu kimapenzi watoto wetu wa kike. Wanadhulumiwa na kufanyiwa mambo hayo bila hiari yao. Ni kwa sababu ya umasikini na kukosa mambo muhimu kama maji ndiposa wanakwenda kule kukubaliana na wanajeshi. Ilionyeshwa wakati mmoja kwenye runinga, watoto wengi wakizungu. Hawa watoto waliachwa humu nchini nao hao wanajeshi Waingereza. Itakuwa vema mazingira maalum yakitengenezwa karibu na kambi zile ili kuwezesha kimaisha jamii zinazoishi mahali pale. Ni muhimu jamii hizo ziwe na maji, hospitali, na shule. Ni muhimu pia watu katika jamii hizo wawe na kazi za kufanya ili isiwe mazoea kwao kwenda kuomba vitu kwenye kambi za wanajeshi. Mwenyekiti wa kamati inayohusika na ulinzi sharti asisitize kwamba kuwepo na taratibu za kuwaruhusu wanajeshi hawa kufanya mazoezi yao humu nchini. Isiwe kwamba tu wakisema wanakuja, sisi hao tunawapokea eti kwa sababu wametuahidi watatufundisha kupambambana na shida tuliyonayo ya ugaidi. Huenda wao ndio watazidisha matatizo! Wanakuja kutufundisha kumpambana na ugaidi. Wanazidisha matatizo kwa sababu hata wale magaidi hawakuwa na haja na sisi Wakenya. Wamekuja hapa wakati fulani kwa sababu Serikali za Marekani na Uingereza ziko hapa."
}