GET /api/v0.1/hansard/entries/691202/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 691202,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/691202/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wekesa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2742,
"legal_name": "David Wafula Wekesa",
"slug": "david-wafula-wekesa"
},
"content": "Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Hii ni fursa ambayo nimeingoja kwa hamu na gamu. Ni ajabu kuwa wenzetu wakiongea, wanafikiri kila mtu ameongea na wanataka kukatiza mjadala. Najua mengi yamehusishwa na huu Mkataba. Haswa ni mambo ya miraa na mengine. Ajabu, inasikitisha kwamba kulikuwa na Kamati ya kuchunguza hali ya mambo ya miraa. Nafikiria huo ndio ulikuwa wakati mwafaka wa hiyo kamati kukaa na Kamati inayohusika na mambo ya ulinzi na mashauri ya nchi za kigeni. Lakini, inasikitisha kwamba wao walipuuza hii Kamati. Nashangaa kusikia Mheshimiwa mwenzangu, Kajuju, akishutumu hii Kamati kwamba ilipuuza maneno yao ama maoni ambayo waliwasilisha kwa hiyo Kamati. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, hata tukiongea zaidi, lazima tuzingatie uhusiano wa jadi ulioko baina ya nchi hizi mbili. Najua kuwa Kenya imenufaika zaidi kutoka Uingereza. Pia, Uingereza imenufaika. Si ajabu Uingereza inahitaji Kenya na Kenya inahitaji Uingereza. Nikiwa mmoja wa walioshiriki kuunda hii Ripoti, sina budi kuiunga mkono. Tulipata nafasi ya kutembelea kambi hizo. Tulikutana na maafisa wahusika. Pia, tulipata fursa ya kukutana na Wakenya ambao wanafanya kazi huko. Walitueleza kwamba uhusiano wao wa kikazi kule ni wa maana na mzuri sana. Vile vile, tukiwa huko, tulipata fursa ya kukutana na Waziri wa Ulinzi. Alitueleza kwa mapana zaidi uhusiano ulioko kati ya hao wanajeshi na wanajeshi wetu na manufaa ambayo wamepata. Vile vile, tulipata nafasi ya kutembezwa Nanyuki na ndugu yangu Mheshimiwa Kimaru, ambaye ni Mheshimiwa wa huko. Tulipata fursa ya kuwahoji watu wa Nanyuki na walituelezea manufaa ambayo wanapata kwa kuweko kwa hao wanajeshi ni ya maana sana. Wakiondoka, ni mengi watapoteza. Kwa hayo machache, sina budi kuunga mkono. Ahsante."
}