GET /api/v0.1/hansard/entries/691390/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 691390,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/691390/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kipyegon",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1453,
"legal_name": "Johana Ngeno Kipyegon",
"slug": "johana-ngeno-kipyegon"
},
"content": "Mhe. Spika, unajua raia wako na shida nyingi sana. Ukisoma jumbe tulizonazo kwa simu, utapata mtu anakuambiaz: “Mtoto wangu yuko hospitalini.” Mwingine anakuambia: “Kuna maiti imekawia kutolewa huko mochari iletwe nyumbani.” Hawana pesa. Mwingine anakuambia: “Mtoto wangu amefukuzwa kwa shule. Hana pesa.” Mwingine anakuambia: “Bw. Spika, wajua sisi hatuna hizo shida kwa sababu tunapata pesa.” Kwa nini tunataka kuwa watu ambao hawataki kusaidiana na wengine? Kwa nini tunakuwa wachoyo hadi kutoa ile kandururu kadogo tunako ndio watu wengine wajimudu ni vigumu? Nilifikiria ninatoka familia ya matajiri, nikiwa kijana mdogo. Lakini ikafika wakati nilikuwa nataka niende ng'ambo kusoma. Wacha nikuambie! Watu walichanga, wakachanga na kuchanga. Wakati nilirudi, kuna mzee mmoja alinionyesha mti aliouza alete kwa mchango wangu. Haukuwa umekatwa. Halafu, unaniambia nikatazwe kuchanga. Hata kama niko na ndururu ama shilingi kumi, pia nitampelekea anayemtuma mtoto ng'ambo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}