GET /api/v0.1/hansard/entries/691391/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 691391,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/691391/?format=api",
"text_counter": 170,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kipyegon",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1453,
"legal_name": "Johana Ngeno Kipyegon",
"slug": "johana-ngeno-kipyegon"
},
"content": "Hatutaki sheria kama hizi. Tuunde sheria inayosaidia Kenya hii. Tunatoka sehemu ambazo watu wanatoa mamilioni ya pesa kila wikendi. Kuna shida gani? Hawa ni watu wameshindwa kufanyia raia kazi. Sisi tumesema: “Kwa sababu wameshindwa kufanyia raia kazi, wacha wazilete hizo pessa kwa michango.” Hivyo, itakuwa tumetumia ile pesa angeleta kufanyia kazi. Napinga hii sheria kabisa. Ningependa hii Nyumba isiwe ya kupitisha sheria mbaya. Tutumie hii Nyumba kujenga nchi yetu. Hakuna hatia kuchanga. Hakuna sheria yoyote kwa hii Nyumba ama kwa Katiba inayokataza na kusema ni hatia kufanya mchango. Uchaguzi unakuja. Utasikia kila hoteli Nairobi hii, iwe Inter-Continental au Laico Regency, Wajumbe wanaunda michango yao ya kuwasaidia kuwania viti. Hata Marekani wanafanya hivyo. Yaani, unataka usaidiwe kuchanga pesa za kwenda kuzunguka kutafuta kiti na hutaki kusaidia mama asiye na hata ndururu ya kupeleka mtoto shule?"
}