GET /api/v0.1/hansard/entries/691945/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 691945,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/691945/?format=api",
"text_counter": 101,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "68(1)(b) cha Kanuni zetu kinatupa nafasi hiyo ya kuamua kwamba Bunge hili liketi kama Kamati Kuu na kujadili jambo lolote kwa kina kirefu na kutoa uamuzi mwafaka. Tumejaribu kutumia Kamati ya Maseneta 11 kwa vipindi vinne. Nashukuru kwamba Kamati zote zilitekeleza wajibu wao ipasavyo, lakini wengine wetu, kwa sababu moja au nyingine, hawakufurahia. Kwa hivyo, kila Seneta apewe nafasi ya kujitapa na kutoa mapendekezo yake kwa jinsi ambayo mwenyewe anafikiria yanahitajika Nyeri. Ninashukuru kwamba mahakama, kwa mara ya kwanza, imekaa kando kidogo, sio kama vile ilivyotekeleza wajibu wake hapo awali kuhusu jambo la kung’atuliwa mamlakani kwa Gavana wa Embu. Kwa kujenga historia ya Seneti, natumai kwamba matokeo ya kamati itakayoundwa yatakuwa ya kupendeza na kukubalika na watu wa Nyeri. Bw. Spika, nashukuru."
}