GET /api/v0.1/hansard/entries/692670/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 692670,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/692670/?format=api",
    "text_counter": 172,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kipyegon",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1453,
        "legal_name": "Johana Ngeno Kipyegon",
        "slug": "johana-ngeno-kipyegon"
    },
    "content": "Najua sheria hii ililetwa kutoka upande ule mwingine. Lakini, tuikatae ikifika hapa, tafadhalini. Hata rafiki yangu Mwenyekiti wa Kamati ya Kiidara ya Haki na Masuala ya Sheria aliyeleta huu Mswada hapa namuuliza autoe. Mhe. Spika, unajua umaskini si kitu unajiitia. Mwenyezi Mungu hajatakia yeyote kuwa maskini. Hakuna mtu Mwenyezi Mungu alimtuma duniani na kumuambia: “Nenda uwe maskini.” Umaskini unaletwa na shida. Shida moja ni kutokuwa na rasilimali. Shida ya pili ni viongozi wanaokataza wananchi kupata au kufikia rasilimali za nchi hii. Kwa sababu tunataka michango iendelee, ile sheria ambayo labda tungekubali ni inayosema michango ifungwe miezi sita au mitano kabla ya uchaguzi. Saa hii, nimechaguliwa na raia. Raia wana shida. Eti naambiwa nisiende kwa michango miezi miwili au sita baada ya kuchaguliwa. Huenda mtoto wa mtu yuko hospitalini. Wengine wanafaa kupelekwa India kwa operesheni halafu tunaambiwa hatuwezi kuwachangia kwa sababu tu Wajumbe! Wewe ni Mjumbe wa nani kama huwezi kusaidia hata mtoto anayepelekwa hospitali? Wewe ni raia aina gani uliye nacho na hutaki kusadia wengine? Napinga. Napinga nikisema lazima turuhusiwe kusaidia watu wetu walio na shida katika nchi hii. Tuko na pesa iitwayo “bursary”. Tunajaribu kugawa hiyo pesa. Ukigawa, unagawa hadi iishe. Lakini, kuna wengine wameshindwa kupata. Wengine wanapata lakini haijatosha kulipia karo. Hapo ndio tunachukua fursa hii tuseme twende tuchangie na kuwalipia. Ningependa niseme napinga huu Mswada. Tunakemea aliyeleta Mswada huu. Atafute Mswada mwingine wa kuleta kwa hii Nyumba. Napinga. Ahsante."
}