GET /api/v0.1/hansard/entries/696133/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 696133,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/696133/?format=api",
"text_counter": 175,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bedzimba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1933,
"legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
"slug": "rashid-juma-bedzimba"
},
"content": "ya Kikristu pia wepelekewe walimu wao ili watoto wetu wakue katika mazingira ya dini, kupendana na huruma. Huo ndio wakati pekee ambapo mtoto akiwa shuleni aone dini imewekwa katika somo, atachukua na uzito. Kulingana na mazingira yaliyoko sasa mitaani, ni vyema sana watoto wetu wapate mafunzo ya kidini. Wanafunzi wakue katika maadili ya kidini kuanzia shule za chekechea, shule za msingi na zile za sekondari. Ikiwezekena, wakati mitihani inapotungwa, wawekewe maswali hayo ili wakifanya mtihani, waone umuhimu wake. Kila siku kabla hawajaingia madarasani, wawekwe katika sehemu za imani zao ili wafundishwe hali halisi jinsi dini inavyosema, aina ya upendo na jinsi ya kuishi pamoja ili wakue katika mazingira hayo na tubadilishe taifa letu. Taifa letu sasa limebadilika. Watu wanagawanyika kikabila na kidini. Wanahitaji neno la Mungu na kuelezewa hali zilivyo ili watoto wetu wainukie katika mazingira mazuri."
}