GET /api/v0.1/hansard/entries/696177/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 696177,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/696177/?format=api",
"text_counter": 219,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Lay",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1022,
"legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
"slug": "joyce-wanjalah-lay"
},
"content": "Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii na vile vile kuunga mkono Hoja hii. Ni muhimu sana kuhakikisha watoto wetu wamepata misingi ya kidini na kielimu. Kuna mambo mengi ambayo watoto wanajifunza kutoka kwa mitandao na kwenye runinga. Wakikosa kuwa na misingi ya kidini, utapata wanapotea kimaisha. Ni kweli katika masomo tunayosoma, tuna masomo ya kidini kama Christian Religious Education (CRE) na Islamic Religious Education (IRE). Lakini ni vizuri ya kwamba watu ambao watakua wanaendesha masomo hayo, wawe ni watu ambao wako tayari katika misingi iliyosimama kwa kidini kama vile mashehe ama waliosomea theologia. Umuhimu wa kuwa na misingi ya kidini ni kuwa inaleta uwezo wa kuwapatia watoto mwelekeo katika maisha. Vile vile, kuna watoto wanaopoteza imani kwa sababu ya mambo yanatokea manyumbani mwao. Kwa wengine, wazazi wao wana matatizo ya ulevi, ama mama zao wanapitia hali ngumu katika ndoa. Wakienda shuleni, watoto hawa hawatulii na kuangazia masomo. Kwa hivyo, wakiwa na walimu wa dini, watoto hao watapata matumaini na misingi ya kuweza kusimama wakijua kuwa mbeleni, kuna maisha bora na vile vile wataweza kutia bidii katika masomo yao. Hoja hii ni ya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}