GET /api/v0.1/hansard/entries/696309/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 696309,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/696309/?format=api",
"text_counter": 100,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Ndiyo, Mhe. Spika. Nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kutoa mchango kwa Mswada huu, ambao umezua hisia tofauti miongoni mwa wananchi na Wabunge. Kama tunavyojua, michango imeisaidia nchi hii, haswa wanafunzi na wagonjwa. Harambee zimetoa mchango wa kutosha katika nchi hii. Shida inatokea mchango unapochukuliwa kuwa kigezo cha uongozi bora, haswa inapodhaniwa kwamba kiongozi ambaye anazunguka nchini akitoa michango mingi ni kiongozi bora kuliko viongozi wengine, bila ya watu kufikiria kuhusu mahali ambapo kiongozi huyo anazitoa fedha hizo. Kuna uzuri wa michango. Ningependa kusema wazi kwamba katika eneo la Pwani, miradi mingi imefanywa kupitia michango. Shule nyingi zimejengwa kupitia michango. Vile vile, watu wamesaidiwa kwenda shule na kufanikisha masomo yao kupitia michango. Watu wamesaidiwa kulipa gharama za matibabu katika hospitali kupitia michango. Hatuwezi tu kuamka leo na kusema kwamba michango haitakuwepo tena. Suala hili ni sharti liangaliwe kwa undani ili tujue linalohitajika kufanyika. Sikatai kwamba kuna watu ambao wametumia michango vibaya. Watu wengine wamefanya michango na kukataa kutoa hesabu. Ni muhimu kuangalia sehemu ya michango inayotumiwa vibaya. Ni muhimu pia tuangalie sheria inayofaa kuwekwa maanani ili ionekane wazi kwamba ikiheshimiwa michango itafanyika kwa njia ya uwazi na wala sio kutapeli. Mhe. Spika, mara nyingi watu wametuma jumbe kwenye runinga au kwenye simu za mikono ama kuandika barua wakiomba michango ya watu wagonjwa au wale ambao wamekufa. Baadaye, ukifuatilia kwa undani utaona kwamba hayo yote ni utapeli, na hamna jambo lolote kama hilo. Tunafaa kuangalia sheria itakayowekwa ili michango isitumiwe vibaya na ili nafasi hii isipotoshe watu na tusinyime wale watu ambao wanahitaji michango nafasi ya kujiendeleza. Mswada huu unafaa kufanyiwa marekebisho kwa kuweka vipengele ambavyo vitahakikisha kwamba wale ambao wataomba michango ni watu ambao wanastahili kupata msaada ili tuhakikishe ya kwamba wanafunzi ambao wanahitaji kusaidika wanasaidika. Tukiwafungia watu wote kwa kupitisha sheria hii basi, watu ambao wana nia nzuri ya kusaidiana na kusaidiwa wataathirika. Tutakuwa tumewanyima nafasi nzuri ya kujiendeleza. Ninavyozungumza hivi sasa, watu wengi wanahitaji matibabu. Mara nyingi tunapopata maombi ya kuwasaidia wale ambao wameathirika, tunakusanyika kama jamii na kuwaita marafiki na kuomba michango kutoka kwao ili tuwasaidie. Mara nyingi watu wanapatwa na ajali The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}