GET /api/v0.1/hansard/entries/696310/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 696310,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/696310/?format=api",
"text_counter": 101,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "za vifo na wanafaa kusafirisha miili ya ndugu zao kutoka Nairobi hadi Mombasa au miji mingine. Mara nyingi tunaitisha michango. Tukiupitisha Mswada huu na kuharamisha michango, tutafanya nini? Sio familia zote zina uwezo wa kugharamia au kufidia gharama za matanga, na ujenzi wa shule na hospitali. Tukifunga michango kwa sheria basi tutawanyima watu hao nafasi ya kusaidiwa na wale ambao wana uwezo. Mara nyingi watu wanakutana na kuchanga kiasi kidogo cha pesa kwa muda fulani, na mwishowe wanaweza kumudu gharama iliyokuwa inawatatiza. Maoni yangu ni kwamba Mswada huu urekebishwe ili watu ambao watachangiwa kwa sababu moja au nyingine waweze kuwajibika na kupeleka ripoti kwa msajili kuonyesha jinsi fedha hizo zilivyotumika, kama itakavyopendekezwa ili watu waone kuwa pesa ambazo zimechangishwa zimetumiwa kwa minajili ambayo ilikuwa inahitajika. Kama ni karo, basi ijulikane kuwa mwanafunzi amechangiwa kiasi fulani cha fedha na fedha hizo zimetumika kwa njia inayostahili. Iwapo ni gharama ya hospitali, basi gharama hizo zigharamiwe na wenyewe watoe stakabadhi za kuonyesha kwamba walichangiwa fedha kiasi fulani na jinsi ambavyo fedha hizo zimetumika. Kama ni fedha za mazishi, basi iwe hivyo hivyo. Ninapinga pendekezo la kuondolewa kwa ujumla mambo ya michango. Msimamo wangu ni kuwa michango iendelee. Tunafaa kuifanyia marekebisho sheria husika kwa kuweka vipengele ambavyo vitawashurutisha wale wanaochangiwa – iwe ni wanafunzi, wagonjwa au makanisa – kutoa stakabadhi zitakazoonyesha kwamba fedha zilizochangishwa zilitumika kulingana na maombi yao. Kwa hayo mengi, naomba kuweka tamati, nikiwaomba Wabunge wenzangu waniunge mkono ili tusije tukalazimika kuunda kamati ya uwiano kati ya Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti ili jambo hili lifanyiwe marekebisho. Naomba Mswada huu upitishwe na wenzangu, tukizingatia suala la kupendekeza mabadiliko."
}