GET /api/v0.1/hansard/entries/696329/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 696329,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/696329/?format=api",
"text_counter": 120,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2308,
"legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
"slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
},
"content": "Asante sana Mheshimiwa Spika. Kuna mtu hapa analia akisema umenihurumia zaidi kwa sababu yeye amebonyeza mbele yangu. Hata hivyo, achana naye. Nataka kuchukua nafasi hii nikushukuru kwa kunipatia wakati huu. Ni fikra yangu kwamba walioleta Mswada huu hawajui wanakoelekea. Mimi naupinga kikamilifu. Mtindo wa Harambee ambao umeletwa na mwanzilishi wa taifa hili, Mzee Jomo Kenyatta, uungwe mkono mia kwa mia na watu waendelee na shughuli hizo kila uchao. Mheshimiwa Spika, wengi hapa hawataki kujieleza lakini tunajua kwamba wamesomeshwa kwa njia ya Harambee. Hata nakumbuka siku moja nilienda Harambee ya Mheshimiwa Duale, tukamchangia kwa sababu hili ni jambo ambalo ni muhimu sana. Kwa hivyo, ikiwa kiongozi wa walio wengi alifanyiwa Harambee, mwingine nani ambaye anaweza kusema ya kwamba Harambee hazifai?"
}