GET /api/v0.1/hansard/entries/696353/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 696353,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/696353/?format=api",
"text_counter": 144,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Pukose",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1458,
"legal_name": "Robert Pukose",
"slug": "robert-pukose"
},
"content": "Asante, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuchangia Mswada huu. Ninaupinga Mswada huu unaosema kwamba tunataka kutupilia mbali mambo ya Harambee. Ninafikiri kuna kasumba mbaya ambayo imeenezwa na watu ambao wana wivu jinsi mwito wa Harambee unavyoisaidia nchi hii kuimarika. Mwito wa Harambee umesaidia watu wengi. Hatufanyi Harambee kwa minajili ya kujisaidia. Tunawafanyia Harambee wale ambao hawajiwezi kwa namna moja au nyingine. Nimeshangazwa na jirani yangu, Mhe. Ferdinard Wanyonyi aliposema hataki Harambee. Mara nyingi yeye hunialika kwenye mikutano ya Harambee katika sehemu yake ya uwakilishi Bungeni. Nimeshangaa kusikia akisema anauunga mkono Mswada huu wa kukomesha shughuli za Harambee. Tunajua kwamba Harambee zimesaidia mambo mengi. Kwa mfano, mwishoni mwa juma lililopita, tulifungua kanisa moja kwenye sehemu yangu ya uwakilishi, katika mahali panapoitwa “Kaibei” kwa sababu kanisa hilo lilijengwa kupitia Harambee. Ningependa Harambee ziendelee ili wale walio na shida za namna moja au nyingine waweze kusaidika. Harambee huwasaidia watoto werevu kutoka jamii maskini kupata elimu, kujenga makanisa na shule, na hata kugharamia matanga na mambo mengine. Kwa hivyo, Sen. Anyang’-Nyong’o anakosea anapoleta Mswada na kutaka Harambee ziharamishwe. Mimi, pamoja na Wabunge wenzangu, nitaupinga Mswada huu kwa vyovyote vile. Mwito wa Harambee ulianzishwa na Hayati Mzee Jomo Kenyatta kwa sababu aliona ungesaidia kuimarisha nchi hii. Hii ni kasumba inayosukumwa zaidi na Wabunge kutoka mrengo wa CORD; na haswa chama cha ODM, ambako Sen. Anyang’-Nyong’o anatoka. Katika Bunge hili, wanachama wa CORD ndio wanaosukuma ajenda ya kuharamisha Harambee. Wakenya wanastahili kuuangalia kwa makini sana kwa sababu haitakuwa vizuri tukiwa na serikali ambayo haitaki wale ambao wanashida wasaidiwe kwa vyovyote vile. Kwa hivyo, ninaupinga Mswada huu."
}