GET /api/v0.1/hansard/entries/696485/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 696485,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/696485/?format=api",
    "text_counter": 276,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "lakini nataka kuwaarifu kuwa miaka iliyopita, KENATCO iliingia katika shida hiyo. Shirika la Kenya Re wakati mmoja liliingia katika shida hiyo. Shirika la Kenya National Assurance nalo likazamishwa hivyo. Jusi tuliona National Bank of Kenya (NBK) nayo inataka kuzama. Kumbuka NBK ilitumiwa wakati ule wa kahawa za Chepkube. Shirika la Kenya Petroleum Refinery Limited limeuzwa hivyo hivyo kiholela na limeenda. Shirika la Kenya Cashew Nuts limeenda. Shirika la Kenya Meat Commission (KMC) mpaka sasa hatujui liko wapi. Mashirika kama Kenya Planters Co-operative Union, Kenya Farmers Association, orodha ni ndefu yamefilisika, na wale ambao wamehusika mpaka sasa wako na tunawajua. Naomba tuliangalie Shirika la KQ tuone ni nini kinalifanya liangamie. Nina ufasaha na uzoefu wa masuala ya fedha na uhasibu. Kitu cha kwanza kuuliza ni kwamba, shirika la KQ linanunua mafuta wapi? Ndilo shirika pekee ambalo linanunua mafuta bila kuungana na mashirika mengine ya ndege kuchangia ununuzi wa mafuta? Ndilo shirika pekee linalonunua mafuta kwa bei ghali kuliko mashirika yote ambayo yanahudumu katika Afrika? Hii ni kwa sababu wanaohusika wanataka wapate hizo fedha wajinufaishe wenyewe. Hilo ni suala la kwanza. La pili, njia ya kutoka Nairobi kwenda Roma iliondolewa kwa KQ? Kwa sababu gani iliondolewa? Hiyo ni moja ya njia ambazo zina faida kubwa sana, lakini likaenda kwa shirika la ndege la KLM. Sote tunaelewa nini kilichotokea. La tatu, fedha ambazo zinaingia kwa shirika hili zina mipango mingi. Tukiangalia hesabu ambayo inatolewa kila mwaka, utakuta mapato, uuzaji na utendakazi. Wazungu wanasema kuwa ‘sales, revenue and operations’. Mapato yake yameendelea kudidimia kwa sababu fedha nyingi zinaelekezwa kwa mikono kadha wa kadha. Kampuni kama Lafarge iko na wakurugenzi kila mahali. Hilo si jambo la kushangaza kwa sababu ni mbinu zilikuwa zimepangwa awali kuangamiza hili shirika. Tukiangalia shirika la KQ lilichukua ndege kwa mkopo. Ndege zenyewe ni Boeing 707, 767 na 787. Ziko wapi baada ya kuzilipia? Baada ya kuzilipia, tulikuwa tunatarajia ndio zitaanza kuleta mapato. Si ukilipia nyumba unakaa na unasema “ Alhamdu lillahi, nimelipa”? Lakini Shirika la KQ liliamua kuuza hizo ndege zote kwa sababu wale wamepatiwa nafasi ya kuongoza hili shirika, nia zao ni tofauti kabisa. Naomba tuanzishe Kamati ambayo itachunguza na tuwache mambo ya siasa ya kuhusisha huyu na yule. Tutafute Wabunge wenzetu. Tunajuana na tunaelewana. Tutafute watu ambao wataleta ufasaha na wataweza kutoa kwa kina ambacho kimefanya hili shirika lipate taabu na shida kiasi cha kwamba litaangamia. Nashukuru hili suala limekuja na naomba Wabunge wenzangu tushikane angalau tuokoe nchi hii yetu kutoka kwa majanga haya, na iwe tutaendelea hivyo hivyo. Shirika hili lilikuwa linachunguzwa na Public Investments Committee na hatimaye Mwenyekiti akasema Seneti ilikimbilia uchunguzi huo. Tukakubaliana na tukasema kuwa hatuwezi kuendelea. Kama si sababu ya Seneti, tungeendelea na uchunguzi."
}