GET /api/v0.1/hansard/entries/696503/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 696503,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/696503/?format=api",
    "text_counter": 294,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nassir",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "hizi fedha hazikuidhinishwa na Bunge ili shirika hili lipewe. Makosa haya haya tunayoyafanya katika shirika hili yamefanywa katika mashirika kama vile Mumias Sugar. Tukiangalia historia ya Kenya, mashirika yaliyopewa kipao mbele kuleta fedha katika nchi hii ikiwemo Nzoia Sugar, Telkom Kenya, Kenya Railways yamedidimia na ukiangalia, hata kwa akili za mtoto mchanga, hii ni mipangilio ya watu ya kuvuja pesa za umma na tunayaregerea. Tuna baadhi ya watu ambao tuko katika Kamati ya Fedha, Mipango na Biashara. Nakumbuka KQ ilileta ombi ili wahifadhiwe wasilipe ushuru wa VAT. Wengine wawe wanalipa lakini wao wasilipe. Shirika hili lilipewa jawabu na Bunge kupitia Kamati ya Fedha, Mipango na Biashara ambayo mimi ni mmoja wa wanakamati, kuwa jambo hilo haliwezi kukubalika. Walielezea Kamati kuwa kuna dalili mbaya zaidi kuwa pesa zitapotea na ninasisitiza jambo hili."
}