GET /api/v0.1/hansard/entries/696849/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 696849,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/696849/?format=api",
"text_counter": 277,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nami nitoe mchango wangu kwa kuunga mkono Ripoti hii ya Mashirika ya Serikali ambayo imetolewa na Kamati ya Uwekezaji. Ripoti hii imeangazia mambo kadha wa kadha kuhusu mashirika ya Serikali. Inafafanua kwa uwazi changamoto ambazo mashirika haya yanapitia. Nitaanza na hali hafifu ya uwajibikaji kwa kitengo cha hesabu za fedha. Uhasibu ni kitu muhimu katika shirika lolote, utendaji kazi wowote ama kampuni yoyote. Inaweza kubainisha waziwazi kama shirika hilo ama kampuni hiyo linaendesha kazi zake kulingana na wajibu wake. Katika mashirika haya yote ambayo yalikuja mbele ya Kamati ya Uwekezaji, ilibainika wazi kuwa mengi yao yalishindwa kabisa kuweka bayana hesabu zao za fedha. Ilionyesha kuwa hapo ndipo kuna njia ambazo zimetafutwa na maafisa wakuu za kupoteza na kuiba pesa za umma. Inasikitisha kuona kuwa katika Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Vitabu vya Serikali, naye pia anashindwa kutoa maoni yake kuhusu hesabu za fedha za kampuni hizo kwa sababu hakuna stakabadhi za kutosha. Hii ni kwa sababu wakiambiwa waziwasilishe hawazisawalishi. Mara nyingi, inakuwa ni changamoto kubwa kwa watu kuweza kubainisha kama makampuni haya yaliundwa ama yalianzishwa na Serikali ili kuhakikisha yanatoa huduma kwa umma ama kufaidi watu binafsi. Utakuta kitengo kama Chuo Kikuu cha Ujuzi cha Kenya ni shirika ambalo linafilisika. Ukiangalia utaona ni shirika la umma. Sababu ni kuwa fedha hazipo za kutosha. Na pale fedha zimetolewa, hakuna uwajibikaji. Suala nyeti ambalo tunajiuliza ni kwamba hao ambao wanateuliwa kuongoza mashirika haya, watakuwa wamekosa nidhamu kwa muda gani ndio wachukuliwe hatua? Tutaendelea na hatua hizi kwa muda gani? Kila mwaka, Bunge hili linaombwa litoe idhini ya fedha kiasi fulani zitolewe ili kuendesha mashirika haya. Lakini fedha zikishaingia, zinatumbukia katika shimo kubwa na hakuna mtu anayewajibika wala anayefuatilia na kuuliza mashirika hayo yanafanya nini. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}