GET /api/v0.1/hansard/entries/696850/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 696850,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/696850/?format=api",
"text_counter": 278,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "La kushangaza ni kuwa utakuta pia wakurugenzi ambao wanatakiwa waendeshe mashirika haya mara nyingi muda wao wa kuhudumu katika mashirika hayo huwa umeisha. Ukishaisha, inachukua muda mrefu sana kuona wengine wameteuliwa. Wale wanahitajika kuhakikisha hawa wakurugenzi wameteuliwa huwa wamelala na kuzembea katika kazi yao. Unakuta mashirika haya yanaendeshwa bila wakurugenzi. Tukiangalia sheria za kampuni, tunaona ziko wazi. Utendajikazi wa kampuni yoyote, mwelekeo wake na mwongozo wake unatolewa na wakurugenzi wakisaidiwa na mkurugenzi mkuu. Kama mkurugenzi mkuu ameachwa peke yake, yeye pamoja na maafisa wake watafanya watakalo, na mara nyingi huwa ni uporaji wa pesa za umma. Pesa za umma zimeporwa na zitaendelea kuporwa. Inasikitisha sana kuona sheria za nchi ambazo ziko wazi, na kila mtu anazijua kama sheria za kulipa ushuru zikivunjwa. Unakuta hata sisi Wabunge katika mishahara yetu, kuna kiwango kinakatwa ama tunatozwa kama kodi - Lipa Vile Ulivyolipwa. Wazungu wanaita PAYE . Unakuta fedha hizo zikitolewa kwa mshahara wa mfanyikazi, mashirika haya hayahakikishi kuwa zimefika kwa Kitengo cha Kodi. Kitengo cha Kodi kinabana kikijua kuwa haya mashirika yana deni. Pesa za wafanyikazi wenyewe huwa zinakatwa ili kulipia vitengo kadha wa kadha kama NSSF na NHIF. Lakini unakuta mara nyingi fedha hizi zinaondolewa kwa mshahara wa mfanyikazi lakini hazipelekwi pale zinapotakiwa ila zinabanwa. Mfanyikazi kesho akiwa anataka huduma ya hospitali anaambiwa kuwa kadi yake haiko sawa kwa sababu hizo fedha hazijapelekwa. Akienda kuuliza anaambiwa hakuna chochote. Ninakumbuka kuna shirika ambalo pia lilikuwa na uzoefu kama huu - Shirika la Reli. Likakata fedha za wafanyikazi hasa za kustaafu. Baadaye shirika lilipokuwa linauzwa, wenyewe ambao wamestaafu wakawa hawana pesa za kuwasitiri wakati wamestaafu, kwa sababu lilikuwa ni deni kubwa kiasi kuwa Shirika la Reli lilikuwa haliwezi kulipa. Kuna mashirika mengi ya Serikali ambayo yako katika janga hilo hilo. Inababaisha na kusikitisha kuona kuwa mashirika yetu ambayo nia ya Serikali kuyaunda ilikuwa iwape wananchi huduma ili angalau maisha yao yabadilike, yamekuwa ni mashirika ya kunufaisha na kutajirisha watu wachache. Katika uwajibikaji wetu kama wanakamati, wakati mashirika haya yamekuja kutoa stakabadhi zao za ardhi, inasikitisha kuwa mara nyingi ardhi hiyo haina stakabadhi. Unauliza wanafanya nini na wanasema kuwa wanangojea kitengo cha ardhi kiwaletee stakabadhi hizo. Ni mara ngapi tumeona mashirika haya yamelazimishwa kununua ardhi ambayo hawahitaji? Unakuta ardhi labda haina stakabadhi ama cheti. Mtu anakuja Nairobi anahakikisha kuwa ardhi hiyo imepata stakabadhi na amepata cheti. Anakimbia kwa shirika hilo na kuiuzia hiyo ardhi ilhali watu wako hapo kwa ardhi. Hakuna mtu anangoja kuangalia kama ardhi hiyo ina watu au la. Mara nyingi, huwa ina watu. Baadaye shirika hilo linageuka na kuwafurusha wale watu kwa sababu wako kwa ardhi ambayo ni yake ilhali hao watu walikuwa hapo tangu jadi. Lakini watu wamefanya ukora, wakaenda wakachukua cheti na kulazimisha shirika hilo kununua hiyo ardhi. Sasa itakuwa ni utata kati ya shirika na wenyeji. Mambo haya yanatakiwa yatatuliwe. Sheria ya kununua vifaa inayoitwa kwa Kiingereza Public Procurement and Asset"
}