GET /api/v0.1/hansard/entries/696917/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 696917,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/696917/?format=api",
"text_counter": 36,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu wa Spika, ninakushukuru kwa nafasi hii ili nami niungane na wenzangu kwa kutuma rambirambi kwa jamaa na marafiki wa marehemu Bamahriz. Huyu shujaa alifanya kazi ya ukombozi wa pili wa taifa letu ambao uliibua vyama kama The National Alliance (TNA), United Republican Party (URP), Jubilee na vyama vingine vyote. Ni kwa sababu ya kazi aliyofanya marehemu Bamahriz. Alikuwa shujaa. Ninakumbuka wakati mmoja Rais Moi alisema: “Huyu Mwarabu ana lugha mbaya sana ya kusumbua watu. Ikiwezekana, anaweza kurudi kwao Yemen.” Sijui Rais Moi alijuaje kwamba marehemu Bamahriz alitoka Yemen. Hata hivyo, Marehemu Bamahriz alisema: “Mimi nataka tupande ndege moja na Rais Moi, tupitie Sudan ya Kusini, tumshushe pale na mimi niende zangu Yemen.” Kutoka siku hiyo, hakuna mtu mmoja aliyezungumzia mambo hayo. Ni dhahiri kwamba viongozi wakiongea, tunafika pahali. Ninashangaa sasa hata waandishi wa magazeti wanasema kwamba Bamahriz ni mtu ambaye hakuogopa chochote. Enzi hizo aliposema tu chama kimoja kinakandamiza Wakenya, alisemekana analeta lugha ya chuki. Alipata tabu na kuwekwa korokoroni. Hata hivyo, mimi ninaamini kwamba hata Yesu alisulubiwa msalabani kwa sababu ya lugha ya kutomheshimu kiongozi aliyekuwa akitawala. Vile vile, Hayati Mzee Jomo Kenyatta na wenzake walienda jela sio kwa sababu ya kuiba, lakini kwa sababu ya kutetea wananchi. Tunaomba Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi."
}