GET /api/v0.1/hansard/entries/697386/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 697386,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/697386/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nassir",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Spika. Nimesimama kuiunga mkono Ripoti hii ambayo ilitungwa mwaka wa 2014 and kuletwa hapa Bungeni mwaka wa 2015. Kwa ufupi, Ripoti hii iliandikwa kulingana na hesabu ya Wakenya iliyofanywa mwaka wa 2009. Katika idadi ya Wakenya ya milioni 38.6, Wakenya milioni 19.15, ambao ni asilimia 50, ni watoto. Katika idadi hiyo ya watoto, milioni 17.66 ni wale walio chini ya umri wa miaka mitano, ambao ni asilimia 20. Watoto milioni 1.92, ambayo ni asilimia tano, ni watoto ambao wako chini ya umri wa mwaka mmoja. Ripoti hii inaonyesha kuwa watoto milioni 8.81, ambayo ni takriban asilimia 46 ya watoto wote nchini Kenya, ni maskini hohehahe. Utafiti huu ambao ulitekelezwa mwaka wa 2012 umedadisi na kuonyesha kuwa Kenya ina watoto milioni 13.6 ambao ni mayatima na maisha yao yamo hatarini. Ripoti hii inataka nchi ya Kenya kuhakikisha kuwa ofisi husika za Serikali zinaangalia afya za watoto wote. Vile vile, Ripoti inataka hali za watoto ambao wako taabani ziangaliwe wakiwa nyumbani. Ni sharti mambo ya kifedha yachunguzwe pia ndiyo kusitokee jambo lolote kuhusiana na usalama. Watoto hawa, kwa njia yoyote ile, wasitukanwe wala kudhulumiwa kimwili. Ripoti hii pia inasema kuwa watoto hawa wasifanyiwe dhuluma za matendo ya chumbani. Kama Bunge, tunapitisha sera kama hii ili Serikali itekeleze. Ni jukumu la Serikali kuhakikisha kuwa yale tunayopitisha hapa yanatekelezwa. Ripoti hii ililetwa Bungeni mwaka wa 2015, na leo tuko mwaka wa 2016. Ndio tunaanza kuijadili. Ninamuomba Mwenyekiti wa wasimamizi wa Bunge kuhakikisha kuwa Ripoti nyingi ambazo Wakenya wanazisubiri, ikiwemo ile ya Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano, zinaletwa hapa tuzijadili ili Wakenya wapate haki yao. Ahsante sana, Mhe. Spika."
}