GET /api/v0.1/hansard/entries/697869/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 697869,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/697869/?format=api",
"text_counter": 280,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, nashukuru kwa nafasi nzuri ili niweze nami kuchangia Hoja hii ya maana ambayo imeletwa na Mwenyekiti wa Elimu, Sen. Karaba. Maswala yaliyozungumziwa hapa na wenzangu yana uzito mkubwa sana. Kwa kweli ukiangalia, nchi inaelekea njia panda ikiwa inatafuta suluhu ya matatizo ya elimu ya watoto wetu. Nilipopata ripoti hii, nilifululiza mpaka ukurasa wa 21, kipengee cha 233. Sehemu ya kwanza ya haki inasema kwamba elimu ni haki ya kikatiba kwa kila mwanacnchi. Elimu ni haki kwa kila mtu kwa mujibu wa Katiba. Serikali yoyote ina jukumu la kuangalia kwamba, jambo hilo linathibitiwa vizuri na wananchi wanategemeo kubwa kielimu. Lakini cha kuhuzunisha ni kwamba taifa letu halijatambua na kuamua kwamba ni haki ya Mkenya kupata huduma inayomfaa kama vile elimu. Bw. Spika wa Muda, nimekuwa nikitazama kipindi hiki cha miaka minne cha Bunge la Kumi na Moja ambacho kinaelekea kuisha, jambo la kuhuzunisha ni kwamba, viongozi walioko serikalini; Rais mwenyewe, Naibu wake na Mawaziri wao na washirika ambao ni wafuasi wa chama, utaona Rais au Naibu wake wakifunga safari; kama juzi Mheshimiwa Ruto ambaye ni Naibu wa Rais alienda sehemu za Ukambani ninakotoka sehemu za Makueni na akawaambia wananchi kwamba ikiwa wanataka maendeleo ni lazima wajiunge na Serikali ya Jubilee ili wapate maendeleo. Tunaona fikira ya Naibu wa Rais ambaye ana jukumu kubwa sana la kutembea katika taifa letu na kuenda sehemu kama hiyo na kuwaambia wananchi wa pale kwamba wao ni Wakenya na wana haki kupata huduma za serikali bila kuzingatia misingi yao ya kisiasa Bw. Spika wa Muda, ukiangalia ukurasa huo huo, na uangalie maneno hayo, utaona kwamba hakuna sheria Kenya ya kusema kwamba ni lazima Mkenya apate masomo na apewe masomo hayo na serikali. Kila mwananchi ana haki kuamua ataenda wapi. Pia, ukiangalia ukurasa wa 25, mstari wa kwanza, inasema kuweka elimu kuwa ya kibinafsi katika taifa lolote, mkutano huu ni wa dunia. Inasema kwamba unadhihirisha kwamba ile huduma inayotolewa na serikali haitafaa wala haitafua dafu kamwe kwa sababu ukiangalia hali ya maswala ya elimu katika taifa letu, iko na mirengo miwili. Jambo la kuhuzunisha ni hilo. Mimi nasema hapa leo kwamba pahali tunaelekea, tunawasha moto katika taifa letu. Hii ni kwa sababu tumeshuhudia walimu wakiandamana na kugoma. Kuna wakati walienda mgomo miezi mitatu. Watoto wa maskini ambao wazazi wao hawajimudu kuwapeleka katika shule za kibinafsi, walikaa nyumbani miezi mitatu. Lakini, watoto wa viongozi kama Maseneta hapa, Wabunge na watu wanaoshikilia nafasi kubwa katika serikali, waliendelea na masomo yao. Bw. Spika wa Muda, ni kwa nini ripoti hii haizungumzii ya kwamba kubinafsisha elimu kunaharibu sehemu kubwa ya elimu? Ni kwa sababu wakati mambo hayo yanaendelea bali tu na kusema kijuujuu kwamba asilimia 10 ya wale walistahili kutetea wale maskini na kupata haki yao ni wale walizungumza kijuujuu tu walimu waangaliwe masilahi yao na kusema hakuna pesa za kuwalipa. Waliozungumza kwa sauti kuu, mimi nikiwa mmoja wao, asubuhi yake nilikamatwa na kushtakiwa kwa sababu nilisema ikiwa walimu hawalipwi pesa ya kutosha, hawatakuwa na chakula. Na yule ambaye The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}